Ziara ya rais wa Marekani Barack Obama nchini Kenya, tume ya uchaguzi nchini Burundi kumtangaza Nkurunziza kama mshindi wa uchaguzi wa hivi karibuni.

Sauti 21:08
Sayari ya dunia
Sayari ya dunia

Katika Makala hii kwa juma hili tunamulika ziara ya rais wa Marekani Barack Obama ambaye kwa juma hili amelakiwa kwa shangwe na hoi hoi kubwa nchini Kenya, katika ziara ya kihistoria, tayari kwa kuongoza pamoja na mwenyeji wake wa nchi hiyo Uhurtu Kenyatta, kongamano la kimataifa kuhusu uwekezaji na ujasiriamali kongamano ambalo limehudhuriwa na wajumbe wapatao elfu tatu ambao ni wawekezaji na wajasiri mali.Nchini Burundi, tume ya uchaguzi kutangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika wiki hii, matokeo ambayo yanampa ushindi Pierre Nkurunziza ushindi, kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu.Nchini Ugiriki wabunge wakutana kuidhinisha mapendekezo mapya ya wakopeshaji wa kimataifa kuhusu kuipa nchi hiyo mikopo zaidi.