MAREKANI-SUDANI KUSINI-USALAMA

Barack Obama ashinikiza pande zinazokinzana Sudan Kusini

Barack Obama, pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, Jumatatu Julai 27 mjini Addis Ababa.
Barack Obama, pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, Jumatatu Julai 27 mjini Addis Ababa. REUTERS/Jonathan Ernst

Akiwa ziarani Addis Ababa, Ethiopia, Barack Obama ameelezea masikitiko yake kuona hali ya kibinadamu nchini Sudan Kusini " inazidi kuwa mbaya " na kutoa wito wa kutia saini haraka kwenye mkataba wa amani.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amewatolea wito Salva Kiir na Riek Machar kufikia makubaliano ya amani "katika wiki ijayo."

Nchini Sudan Kusini, " hali inaendelea kuzorota, hali ya kibinadamu ni mbaya ", amesema rais Barack Obama katika mkutano na waandishi wa habari mjini Addis Ababa, baada ya mkutano baina yake na waziri mkuu wa ethiopia, Hailemariam Desalegn. Rais wa Marekani ametoa wito wa kutia saini kwenye mkataba wa amani "ndani ya wiki moja " kati ya pande zinazokinzana.

Pendekezo la IGAD laungwa mkono

Wito ambao unafanana na ule wa IGAD, uliotolewa Jumamosi Julai 25. Mamlaka ya Maendeleo ya Afrika Mashariki, inayohusika na upatanishi kati ya rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, imetoa rasimu ya mkataba ili kurejesha amani nchini Sudan Kusini. Wapatanishi wa kimataifa wanaomba mkataba wa amani utiliwe saini kabla ya Agosti 17. Mazungumzo hayo kutoka pande zote mbili yanatarajiwa Ijumaa Julai 31 mjini Addis Ababa ili kufahamishwa kuhusu nakala hiyo, kabla ya kuanza kwa mazungumzo yaliopangwa kufanyika Agosti 5.

Tatizo linalosalia ni lile la uwezo kwa wahusika mbalimbali, ikiwa ni pamoja na IGAD. Lakini Barack Obama amesema, baada ya mwaka mmoja na nusu wa migogoro, vita vya wenyewe kwa haviwezi kuendelea. Rais wa Marekani ameahidi vikwazo vipya, iwapo mapendekezo ya IGAD yatafeli.