MALI-SHAMBULIO-USALAMA

Kambi ya jeshi kaskazini mwa Mali yashambuliwa

wanajeshi wa Mali, hapa ni katika mji wa Goundam, karibu na Tombouctou.
wanajeshi wa Mali, hapa ni katika mji wa Goundam, karibu na Tombouctou. AFP/PHILIPPE DESMAZES

Kambi ya jeshi la Mali imeshambuliwa katika jimbo la Tombouctou. Watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi wameendesha mashambulizi mapema Jumatatu asubuhi wiki hii, na kushikiliwa kwa masaa kadhaa kambi ya kijeshi ya Gourma Rharous kaskazini mwa Mali. Wanajeshi kumi wanasadikiwa kuuawa katika shambulio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea mapema Jumatatu asubuhi wiki hii. Watu wenye silaha wameendesha shambulio katika kambi ya kikosi cha wanajeshi wa ulinzi wa taasisi za nchi katika mji wa Gourma Rharous. Mji unaopatikana kwenye umbali wa kilomita 120, mashariki mwa jimbo la Tombouctou.

Wauaji hao hawakuweza kujulikana, lakini inashukiwa kuwa huenda wakawa wapiganaji wa kiislamu. Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, makundi mengi yalionekana tangu katikati mwa mwezi Julaia katika eneo la shambulio.

Mazingira ya usalama yaleta utata

Shambulio hili limesababisha vifo vya watu kumi. Idadi hii ni kubwa kwa jeshi la Mali tangu mwezi wa Januari. Wanajeshi wa Mali wamnejielekeza mara moja katika mji wa Gourma Rharous ili kukabiliana na watu hao. Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita, wanajeshi wengine wawili wa Mali waliuawa katika shambulio la kuvizia katika eneo la Nampala, kwenye mpaka na Mauritania.

Katika uwanja wa vita, mapigano yanaendelea licha ya mkataba wa amani kutiliwa saini Mei 15 na upande wa serikali, huku kambi ya waasi ikitia saini kwenye mkataba huo Juni 20.