COTE D'IVOIRE-SIMONE-SHERIA

Côte d'Ivoire: Anselme Seka Yapo ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Baada ya kuahirishwa mara kadhaa, Jumanne wiki hii mahakama ya kijeshi mjini Abidjan imemuhukumu Anselme Seka Yapo, mkuu wa zamani wa kikosi cha ulinzi cha Simone Gbagbo, mwanamke wa rais wa zamani wa Côte d'Ivoire, kifungo cha miaka ishirini jela kwa kosa la mauaji.

Anselme Seka Yapo, mkuu wa kikosi cha usalama cha Simone Gbagbo, mkee wa zamani wa rais wa rais Laurent Gbagbo, ni mmoja wa maafisa wanaotuhumiwa kosa la uhalifu wa wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi.
Anselme Seka Yapo, mkuu wa kikosi cha usalama cha Simone Gbagbo, mkee wa zamani wa rais wa rais Laurent Gbagbo, ni mmoja wa maafisa wanaotuhumiwa kosa la uhalifu wa wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi. AFP / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Anselme Seka yapo amehukumiwa na maafisa wengine saba wa rais wa zamani Laurent Gbagbo kwa kosa la ukiukwaji lililofanywa wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2010-2011.

Miaka ishirini gerezani ni uamuzi uliotangazwa na mwendesha mashtaka katika mahakama ya kijeshi dhidi ya Seka Yapo Anselme kwa uhalifu uliofanywa wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi.

Ingawa amefutiwa makosa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na vifaa vya kijeshi, kosa la mauaji kwa kukusudia ndilo limepelekea anachukuliwa hukumu hiyo.

Anselme Seka Yapo amekutikana na hatia ya kuua kwa risasi dereva wa waziri wa zamani wa Haki za Binadamu, Joel N'Guessan, wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka2011. vipimo vya kinasaba vilibaini kuwa dereva huyo alipatikana aliuawa kwa kuchomwa moto.

Siku moja kabla ya uamuzi, kamishina wa serikali Ange Kessi alidai wakati wa mashitaka yake, kifungo cha maisha kwa yule aliyemtaja kulingana na maneno yake "kiongozi kigogo aliyeweza kuua watu wengi".

Mbele ya majaji, mkuu wa zamani wa kikosi cha usalama cha mkee wa rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo ameonekana mpole wakati hukumu ilipotangazwa.

Kamanda Abéhi Jean Noel ambaye ameripoti mahakamani sambamba na Anselme Seka Yapo amehukumiwa kifung cha miaka mitano jela kwa kosa utoro na kukimbilia ugenini.