COTE D'IVOIRE-UCHAGUZI-SIASA

Côte d'Ivoire: Ouattara awasilisha fomu yake ya kuwania kiti cha urais

Nchini Côte d'Ivoire, Alassanne Ouattara, rais anaye maliza muda wake na mgombea wa muungano wa RHDP unaovishirikisha vyama vinne ikiwa ni pamoja na PDCI na RDR, amewasilisha rasmi fomu ya kuwania katika kiti cha urais.

Alassane Ouattara, rais wa Cote d'Ivoire, amejiorodhesha rasmi kama mgombea urais wa mwezi Oktoba, Jumatano Agosti 5mwaka 2015.
Alassane Ouattara, rais wa Cote d'Ivoire, amejiorodhesha rasmi kama mgombea urais wa mwezi Oktoba, Jumatano Agosti 5mwaka 2015. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Baada ya muhula wa kwanza rais huyo anawania muhula mya wa miaka mitano. Rais Alassanne Ouattara amejiorodhesha rasmi Jumatao Agosti 5 kwenye Tume huru ya uchaguzi CEI.

Alassanne Ouattara ambaye anataka kuchaguliwa kuwa rais katika duru ya kwanza ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba, amekua mtu wa pili kwa kuvuka milango ya Tume huru ya Uchaguzi (CEI) kwa kuwasilisha fomu yake.

Baada ya Eloi Bolou Gouali mgombea binafsi, Alassane Ouattara amewasili Jumatano Agosti 5 akiambatana na baadhi ya wajumbe wa serikali yake kwenye makao makuu ya Tume huru ya uchaguzi ambapo aliwasilisha nyaraka muhimu kwa ajili ya usajili wake kama mgombea.

Ndani ya saa moja nyaraka zote zainazohitajika zilikabidhiwa Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi, Youssouf Bakayoko. Baada ya maneno machache kuhusu hatua hiyo, rais mgombea alienda kukutana na umati wa wafuasi wake waliokua wamekuja kumuunga mkono kwa ajili ya tukio hilo.

" Hii ni siku ya kipekee kwa kwetu sisi. Tumekuja kumuonesha rais kuwa tuko pamoja naye. Mpinzani mkubwa wa rais wetu ni asilimia. Ni kutokana na hali hiyo ambayo imetupelekea sisi sote kuja hapa kuonesha ulimwengu kwamaba hata kama rais Ouattara atakupoa na washindani kumi, anapaswa tu kupata asilimia kubwa. Hakuna swali la duru ya pili. Wanasema " tako Kélé ", ina maana mtoano. Ni pigo la KO! ", amesema mmoja wa wafuasi wa rais Alassanne Ouattara, huku akipongezwa kwa kicheko na wafuasi wenzake.

Tarehe ya mwisho ya usajili itakuwa Agosti 25. Kisha mafaili yatatumwa kwenye Baraza la Katiba, ambalo lina wiki moja ili kusahihisha fomu za wagombea. Mwanzoni mwa mwezi Septemba orodha kamili ya wanaume na wanawake ambao wanatarajiwa kuwania kinyanga'nyiro katika uchaguzi wa urais itakua imejulikana.