MALI-SHAMBULIO-USALAMA

Mali: afisa wa kijihadi akiri kuhusika na shambulio katika hoteli Byblos

Kuta za Hoteli Byblos mjini Sévaré uliharibiwa na risasi baada ya mashambulizi ya kijeshi.
Kuta za Hoteli Byblos mjini Sévaré uliharibiwa na risasi baada ya mashambulizi ya kijeshi. AFP PHOTO / STRINGER

Kiongozi wa juu wa kijihadi aliye karibu na mhubiri Amadou Koufa amekiri Jumanne Agosti 11 kihusika na shambulio katika hoteli moja ya mji wa Sévaré, nchini Mali. Kwa mujibu wa mtu huyo shambulio dhidi ya hoteli Byblos liligharibu maisha ya watu 15, wakati ambapo ripoti rasmi inaeleza hadi sasa kuwa shambulio hilo liligharibu maisha ya watu 13.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2012, mwanajihadi huyo alikua katika kundi la wapiganaji wa Mokhtar Belmokhtar.

Suleiman Mohamed Kennen ni moja ya majina ya kivita ya mwanajihadi huyo. Amekiri shambulio la wiki iliyopita, Agosti 7, katika mji wa Sévaré dhidi ya "maadui wa Uislamu," amesema. Ni mshirika wa karibu wa mhubiri mwenye msimamo mkali nchini Mali, Amadou Koufa, ambaye ndoto zake nia kuweka sheria za kiislamu katika kanda nzima ya Mopti.

Mtu huyo amethibitisha kuwa operesheni hiyo ilibarikiwa na Amadou Koufa mwenyewe, ambayo " hajaonekana hadharani " kwa miezi kadhaa. Amadou Kufa, mwenyewe, katika mkanda uliorekodiwa, miezi michache iliyopita, alitoa wito wa kupambana dhidi ya vikosi vya kigeni nchini Mali.

Uhusiano na Mokhtar Belmokhtar

Lakini mtu aliyedai kuendesha mashambulizi pia ni mshirika wa karibu wa Mokhtar Belmokhatar, na ambaye pia ni mwanajihadi kutoka Algeria. Kwa hiyo inawezekana kwamba timu iliyoendesha operesheni hiyo wiki iliyopita katika mji wa Sevare ilitekeleza kwa amri yake / au shambulio hilo lilitekelezwa na wanajihadi kutoka maeneo ya kaskazini mwa Mali.

Viongozi wa Mali hawajaelezea lolote kuhusu madai hayo, lakini waziri mmoja amesikika akizungumza kwamba shambulio hilo lililoendeshwa katika mji wa Sévaré, nchini Mali lilitekelezwa na magaidi.