SUDANI KUSINI-KIIR-MACHAR-MAZUNGUMZO-USALAMA

Serikali ya Sudan Kusini yakataa kutia sahihi kwenye mkataba

Serikali ya Sudan Kusini imekataa kusaini mkataba uliotarajiwa kuleta amani na kumaliza mapigano yaliyodumu nchini humo kwa zaidi ya miezi ishirini. Lakini waasi na makundi ya upinzani wamesaini mkataba huo.  

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) watafikia kusaini makubaliano ya kuunda serikjali ya mpito ya miaka miwili na nusu?
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) watafikia kusaini makubaliano ya kuunda serikjali ya mpito ya miaka miwili na nusu? REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Serikali imeomba kuongezewa siku kumi na tano zaidi kushauriana juu ya mapendekezo ya kusaini mkataba huo.

Waziri kutoka Uingereza anayesimamia maswala ya Afrika ameitaka serikali ya Sudan Kusini kusaini mkataba huo haraka iwezekanavyo.

Jumatatu Agosti 17 ilikua tarehe ya mwisho iliotolewa kwa pande zinazohusika katika mgogoro unaoendelea nchini Sudan Kusini kwa kusaini mkataba na kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe viliodumu miezi 20 sasa.

Hati iliyopendekezwa na IGAD, taasisi ya kikanda inayosimamia upatanishi kati ya pande zinazopigana nchini Sudan Kusini, imepingwa na pande mbili husika katika mazungumzo, ikiwa ni pamoja na mambo yake ya kisiasa na kijeshi.

Marais wa Ukanda huo, ikiwa ni pamoja na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Omar al-Bashir wa Sudan wamehudhuria mazungumzo hayo yaliofanyika nchini Ethiopia kwa minajili ya kutafuta jinsi ya kupatia ufumbuzi machafuko hayo. Wakati huo huo rais wa Sudan Kusini Salva Kiir hatimaye ameamua kujielekeza Ethiopia kushiriki katika mazungumzo hayo.

Mambo matatu yalikua yanatabiriwa kwa siku ya leo. Jambo la kwanza ni lile la rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar kuona wanasaini mkataba utakaopelekea kuuundwa kwa serikali ya mpito ya mika miwili na nusu. Hati iliyoandaliwa na IGAD, inaeleza jinsi gani serikali hiyo itakavyoundwa, ingawa inaweza kufanyiwa marekebisho kama marekebisho yatakubaliwa na pande zote husika.

Njia nyingine za kuondokana na mgogoro huo

Kama mkataba hautasainiwa, basi kuna uwezekano wa kutumia njia nyingine, ambayo ni ile ya muda uliotolewa kwa pande husika. Lakini jumuiya ya kimataifa imekata tamaa na ukosefu wa nia ya pande zinazopigana ambazo hazijawahi kuheshimu makubaliano saba ya kusitisha mapigano ziliosaini.

Njia ya tatu ambayo inawezekana leo: kila moja anatambua kushindwa kwa mazungumzo katika hali yake ya sasa na wanatafakari kuhusu njia mpya ya kutatua mgogoro huo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tayari lilitangaza vikwazo vitakavyowalenga baadhi ya viongozi, lakini pengine huenda vikwazo hivyo vikachukua muda mrefu wa kusitisha mapigano wakati ambapo pande mbili husika zinabaki tu na uwezo wa kucukua uamzi.