MAREKANI-SUDANI KUSINI-USALAMA

Marekani yamtaka Salva Kiir kusaini mkataba wa amani

Marekani imeitaka serikali ya Sudan Kusini kutia saini mkataba wa amani baada ya siku 15 kama ilivyoahidi ili kumaliza miezi 20 ya mapigano katika taifa hilo.

Mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya watu wengi. Hapa ni pembezoni mwa barabar inayoingia katika mji wa Bentiu, Sudan Kusini, Aprili 20 mwaka 2014.
Mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya watu wengi. Hapa ni pembezoni mwa barabar inayoingia katika mji wa Bentiu, Sudan Kusini, Aprili 20 mwaka 2014. REUTERS/Emre Rende
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo ulitiwa saini na kiongozi wa waasi Riek Machar huku rais Salva Kiir akiomba siku 15 kurudu nyumbani kwenda kushauriana na wenzake kabla ya kurejea tena jijini Addis Ababa kusaini mkataba huo.

John Kirby msemaji wa mambo ya nje amesema Marekani amesikitishwa na hatua ya rais Kiir kutotia saini mkataba huo.

Msululishi wa mgororo huo Seyoum Mesfin  amasema kuwa licha ya serikali kutotia saini mkataba huo, hatua kubwa imepigwa kuelekea kupata amani.

Suala tata limekuwa ni namna ya kugawana madaraka kati ya Machar na Kiir na mkataba uliotiwa saini na Machar na Katibu mkuu wa chama cha SPLM Pagan Amum, unamrudisha Machar katika wadhifa wa Makamu wa rais wa nchi hiyo.