MALI-AZAWAD-MINUSMA-USALAMA

Waasi wa Azawad waiomba Minusma kuondoka Kaskazini Mashariki mwa Mali

Askari wa Minusma wakipiga doria katika mji wa Kidal, Julai 23, 2015.
Askari wa Minusma wakipiga doria katika mji wa Kidal, Julai 23, 2015. REUTERS/Adama Diarra

Siku moja baada ya serikali ya Mali kukosoa utaratibu wa Minusma kutenga eneo maalum ya usalama karibu na mji wa kidal, sasa ni zamu ya waasi wa Azawad (CMA) kuomba askari hao wa kulinda amani kuondoa uamuzi wao huo kaskazini mashariki mwa Mali, na katika maeneo yote mengine ya nchi.

Matangazo ya kibiashara

Eneo hilo maalum la Usalama linakaribiana na ngome ya waasi wa Tuareg, inayopatikana kwenye umbali wa zaidi ya km 1,500 kaskazini mwa mji wa Bamako

Eneo hilo maalum la Usalama ilitengwa baada ya siku tatu ya mapambano na waasi hao tarehe 15 na 16 na 17 mwezi Agosti mwaka huu.

Hivi karibuni serikali ya Mali ilielezea wasiwasi wake kufuatia hatua zilizochukuliwa na vikosi vya Umoja wa mataifa vya kulinda amani nchini Mali (Minusma) kwa kutenga eneo la kilomita mraba 20 kukabiliana na hali ya usalama katika mkoa Kidal.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinatazamia pia kulinda wakaazi wa eneo hilo ambapo makundi ya waasi wa Azawad na wengine yanasababisha ukosefu wa usalama licha ya makubaliano ya amani yaliyosainiwa miezi miwili iliyopita.

Hatua hiyo inaighadhabisha serikali ya Bamako kwa kuchukuliwa bila ya kushauriana baina ya serikali ya nchi na vikosi hivyo.

Umoja wa Mataifa kwa upande wake umesema umewatuma wanajeshi wake katika mji wa Kidal, Kaskazini mwa Mali. Uamzi huu umechukuliwa ili kuzuia kuenea kwa mapigano ambayo yamesababisha vifo vingi Jumatatu Agosti 17 kilomita 120 na mji huo, mapigano ambayo yalizuka kati ya makundi hasimu, Umoja wa Mataifa umeendelea kusema.

Mbali kidogo, kaskazini mwa mji wa Kidal, katika mji wa el-Gerer, eneo lingine ambapo makundi hasimu yamekua yakiendelea na mapigano kwa muda wa siku tatu, hali ya utulivu imerejea, lakini hali ya taharuki imeendelea kutanda, kwa mujibu wa chanzo cha kigeni, ambacho kinahofu ya kutokea kwa mapigano mapya.

Mjini Bamako, baadhi ya maafisa wa serikali wanasema kughadhabishwa na ukiukwaji wa mkataba wa usitishwaji mapigano unaofanywa na washirika wao ambao wamekua wakiendesha vita dhidi ya waasi wa Azawad , viongozi hao wamekumbusha kwamba hivi karibuni rais Ibrahim Boubacar Keita amekuatana kwa mazungumzo kwa muda mrefu na wawakilishi wa waasi wa Azawad na kuwaeleza nia yake ya kuheshimu ahadi zake.