UFARANSA-MOROCCO-UANDISHI-HAKI

Waandishi wa habari wawili wakamatwa Ufaransa

Waandishi wa habari wawili wa Ufaransa wamekamatwa Alhamisi wiki hii mjini Paris. Wanatuhumiwa kutaka kupewa kiasi cha zaidi ya dola milioni 3 kwa kutochapisha kitabu ambacho kilikuwa na taarifa za kutatanisha.

Mfalme wa Morocco, Mohamed VI, Juni 19, 2015.
Mfalme wa Morocco, Mohamed VI, Juni 19, 2015. REUTERS/Maghreb Agence Press/Pool
Matangazo ya kibiashara

Historia hii ilianza Julai 23. Siku hiyo, mwandishi wa habari Eric Laurent aliwasiliana viongozi wa Morocco na kuwafahamisha kuwa anaanda kuchapisha kitabu kuhusu Morocco. Mkutano ulifanyika siku chache baadaye mjini Paris kati ya mwandishi wa habari na wakili wa mfalme wa Morocco. Wakati huo Eric Laurent alipendekeza apewa dola milioni 3 ili asiwezi kuchapisha kitabu hicho. Lakini viongozi wa Morocco walimfungulia mashataka mwaandishi huyo wa habari nchini Ufaransa na uchunguzi wa awali umefunguliwa na Ofisi ya mashitaka mjini Paris.

Vikao vingine vilifanyika ofanyika, lakini wakati huo chini ya usimamizi wa wachunguzi. Na leo, waandishi hao wa habari wawili wako mikononi mwa polisi kufuatia moja ya vikao hivyo ambapo walikubali kupewa pesa.

"Ujasiri ulio na wazimu! "

Mwanasheria wa Ufalme wa Morocco, Eric Dupond-Moretti, kwenye runinga ya RTL, amesema kushangazwa na utaratibu uliotumiwa. “ Nafikiri kwamba ni mara ya kwanza, kwa uwelewa wangu mtu kama mwaandishi wa habari kua na mwenendo kama huo wa kufanya kumsaliti rais aliye madarakani. Hii haijawahi kuonekana, Ni ujasiri ulio nawazimu. Tunajiuliza sababu gani iliyopelekea mwaandishi huyo anafanya hivyo. Je, ni ushujaa? Au mwanaume huyu na mwanamke huyu walifanya hivyo kwa kutumiwa na kundi la watu, na hasa, tumekua tukijiulizala huenda ni suala la ugaidi. Nasema kwa umakini sana, na uchunguzi ndio utakaoamua ", amesema Dupont-Moretti.

Eric Laurent na Catherine Graciet walishawahi kuchapisha kitabu kuhusu Mfalme Mohammed VI mwaka 2012. kitabu kilioitwa Predator kinaelezea waandishi wawili waliomfungulia mashitaka Mfalme wa Morocco.