DRC-USALAMA

Jeshi la DRC lawapoteza wanajeshi wake sita

Rais Joseph Kabila akiwa ziarani Goma, Jumamosi Novemba 30, 2013, aliwataka raia kushirikiana na vikosi vya usalama na ulinzi kwa kudumisha usalama..
Rais Joseph Kabila akiwa ziarani Goma, Jumamosi Novemba 30, 2013, aliwataka raia kushirikiana na vikosi vya usalama na ulinzi kwa kudumisha usalama.. REUTERS/Kenny Katombe

Wanajeshi 6 wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wameuawa katika shambulio la kushtukiza linalodaiwa kutekelezwa na waasi wa kihutu wa Rwanda wanaopigana mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili limetekelezwa kwenye mji wa Rugari kaskazini mwa jimbo la Kivu, mji ulioko umbali wa kilometa 30 na mji wa Goma.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa watu wenye silaha walishambulia gari moja la askari wa DRC wilayani Rutshuru, ambapo wameongeza kuwa wapiganaji hao ni wale waliopiga kambi kwenye mpaka wa nchi hiyo, Rwanda na Uganda.

Wanaharakati wa haki za binadamu mashariki mwa DRC wamesema kukerwa na mdororo wa usalama unaoendelea kushuhudiwa mashiriki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hususan katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Mkoa huo umeendelea kukumbwa na mashambulizi ya hapa na pale yanayoendeshwa na makundi yenye silaha. Makundi mengi yenye silaha kutoka nchi jirani na yale yanayoundwa na raia wa Congo wenyewe yamepiga kambi katika mkoa huo.

Raia wengi wameuawa katika mashambulizi yanayoendeshwa na makundi hayo