DRC-HAKI-SHERIA

DRC: askari 12 wahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela

Muathirika anayedaiwa ubakaji atoa ushahidi wake mbele ya Mahakama ya kijeshi mjiniinayoendesha kazi yake katika mji wa Minova kwa muda wa wiki moja kuwasikia waathirika wa maeneo hayo.
Muathirika anayedaiwa ubakaji atoa ushahidi wake mbele ya Mahakama ya kijeshi mjiniinayoendesha kazi yake katika mji wa Minova kwa muda wa wiki moja kuwasikia waathirika wa maeneo hayo. James Songa, membre Avocats sans frontières Belgique

Mahakama ya Kijeshi ya Beni-Butembo, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya congo, DRC imewahukumu askari kumi na mbili wa jeshi la serikali ya nchi hiyo FARDC, kifungo cha miaka ishirini jela, kwa makosa ya ubakaji na mauaji.

Matangazo ya kibiashara

Hukumu hiyo ilitangazwa na Mahakama hiyo mwishoni mwa juma lililopita mjini Kasindi-Lubiriya, ulioko kwenye umbali wa kilomita 75 kaskazini mwa mji wa Beni mkoani kivu kaskazini.
Wakaazi wa Kasindi wamekaribisha hatua hiyo ya mahakama kufwatia kile walichokisema wengi baadhi ya askari wa jeshi hilo, wanawadhalilisha wananchi bila kujali haki za kimsingi za kibinadamu.

Jumla ya watuhumiwa kumi na nane ikiwa ni pamoja na askari watano wa FARDC na maafisa watatu wa polisi walishitakiwa na mwendesha mashitaka wa kijeshi kwa makosa ya ubakaji na mauaji.

Hayo yakijri watetezi wa haki za binadamu Wilayani Beni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanawashtumu vijana katika wilaya hiyo wanaojiiita Mai Mai kushirikiana na waasi wa ADF Nalu kupambana na jeshi la serikali na kuwavamia raia.