Pata taarifa kuu
MISRI-MAUAJi-USALAMA

Misri: watu 12 ikiwa ni pamoja na raia wa Mexico wameuawa

Askari wa Misri Agosti 6, 2015 katika bandari ya Ismailiya.
Askari wa Misri Agosti 6, 2015 katika bandari ya Ismailiya. AFP/AFP/Archives
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Polisi na jeshi la Misri wamewaua watu 12 Jumapili mwishoni mwa juma hili, ikiwa ni pamoja na watalii kutoka Mexico na raia wa Misri, wakiyalenga kwa makosa magari yao wakati walipokuwa wakiwatimua wanajihadi magharibi mwa Misri.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Mexico imethibitisha vifo vya raia wake wawili.

Jangwa la magharibi, maarufu kwa watalii, pia ni moja ya maficho muhimu ya makundi ya kijihadi, ikiwa ni pamoja na tawi la kundi la Islamic State (IS), linaloendesha mashambulizi kadhaa dhidi ya vikosi vya usalama katika nchi nzima.

" Vikosi vya pamoja vya polisi na jeshi, ambavyo vilikua vikiwatimua magaidi katika eneo la Wahat katika Jangwa la Magharibi, walirusha risasi kwa makosa dhidi ya magari mawili madogo (pick-up) yaliokuwa yakisafirisha watalii kutoka Mexico ", wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema katika taarifa yake.

" Watu kumi na wawili waliuawa na 10 kujeruhiwa miongoni mwa watalii kutoka Mexico na Wamisri" ambao waliandamana nao ", imeongeza wizara ya mambo ya ndani, huku ikibaini kwamba raia hao walikuwa katika eneo ambalo " hairuhusiwi kwa watalii. "

Hata hivyo wizara ya mambo ya ndani ya Misri haijataja idadi ya raia wa Mexico waliouawa au ni aina gani ya silaha iliotumiwa kwa kurusha risasi dhidi ya magari yao.

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Mexico amethibitisha haraka vifo vya watalii wawili kutoka Mexico, akiongeza kuwa watu wengine watano waliojeruhiwa katika shambulio hilo wamelazwa katika hospitali ya mjini Cairo, ambapo wanaendelea vizuri.

Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto amelaani shambulizi hilo kwenye akaunti yake ya Twitter, akitolea wito Cairo kuanzisha "uchunguzi wa kina".

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.