Dhana ya demokrasia na uelewa wake katika baadhi ya nchi za Afrika mashariki na kati

Sauti 16:06

Jumanne ya septemba 15 dunia iliiadhimisha siku ya kimataifa ya demokrasia, lengo likiwa ni kusherehekea mafanikio ya demokrasia, lakini vilevile umuhimu wa kuiendeleza na kutunza demokrasia kwenye mataifa ya Afrika, kwani bila demokrasia ya kweli maendeleo ni sawasawa na ndoto.Maadhimisho hayo yamefanyika huku baadhi ya nchi zikikabiliwa na changamoto mbalimbali za usitawi wa demokrasia katika nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na siasa, Utawala bora na haki za binadamu.Katika makala haya tunadadavua umuhimu wa demokrasia, na kuhoji je ni kweli demokrasia yenyewe kama inavyozungumziwa iko kwenye mataifa yetu haya ya Afrika Mashariki mna kati?Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kusikiliza makala haya.