MSUMBIJI-SIASA-USALAMA

Msumbiji: mvutano waibuka kati ya vyama vya Frelimo na Renamo

Vue de Maputo, capitale du Mozambique.
Vue de Maputo, capitale du Mozambique. Wikimedia

Mvutano wa kisiasa kati ya vyama viwili vikubwa nchini Msumbiji vinavyounda Serikali vya Frelimo na Renamo, umeendelea kushika kasi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo wanasiasa wa vyama vingine vya upinzani pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu wamewataka viongozi wa vyama hivyo kupata suluhu.

Haya yanajiri wakati huu kukiripotiwa makabiliano ya risasi kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa Renamo, hali inayohatarisha kuvunjika kwa mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya chama cha Renamo na aliyekuwa rais wa msumbiji aliyemaliza muda wake Armando Guebuza.

Tayari makundi mbalimbali kutoka vyama vingine vidogo vya upinzani, wanaharakati na wananchi wamejitokeza kushinikiza wanasiasa wa vyama hivyo viwili kurejea kwenye meza ya mazungumzo na kumaliza tofauti zao, kabla ya kusababisha nchi hiyo kutumbukia kwenye machafuko zaidi.

Lutero Simango ni mkuu wa chama cha upinzani cha MDM ambaye anaunga mkono upatikanaji wa suluhu baina ya vyama hivyo viwili.

Mvutano huu unaripotiwa ikiwa ni siku chache tu zimepita toka, msafara wa kiongozi mkuu wa upinzani na rais wa chama cha Renamo, Alphonso Dlakama ushambuliwe kwa risasi na yeye kunusurika kwenye shambulio hilo.