Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA-USALAMA

Burkina Faso: Macky Sall akutana na jenerali Gilbert Diendéré

Jenerali Gilbert Diendéré amemkaribisha Rais wa Senegal na mMwenyekiti wa ECOWAS alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou, Septemba 18 2015.
Jenerali Gilbert Diendéré amemkaribisha Rais wa Senegal na mMwenyekiti wa ECOWAS alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou, Septemba 18 2015. AFP PHOTO / AHMED AUOBA
Ujumbe kutoka: RFI
3 Dakika

Baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Alhamisi, Septemba 17, wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP) bado wapo katika mji wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuwepo kwa wanajeshi hao, waandamanaji walikusanyika katika uwanja wa ndege kuipokea timu ya upatanishi na kuikumbusha kwamba wanapinga uamzi wa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais wa kufanya mapinduzi ya kijeshi.

Wakati huo huo, RFI imegundua kwamba Rais wa Senegal Macky Sall, pia Mwenyekiti wa ECOWAS, amekutana na jenerali Gilbert Diendéré. Kuhusu kuachiliwa huru kwa Rais Kafando, bado haijajulikana.

Rais wa Senegal Macky Sall amekutana kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi, Gilbert Diendéré, amearifu mwandishi wa RFI, Guillaume Thibault, ambaye yuko mjini Ouagadougou. Macky Sall amewasili mjini Ouagadougou Ijumaa mchana wiki hii. Macky Sall ameambatana na waziri wa mambo ya njei, mshauri wake wa masuala ya kidiplomasia na mkuu wa majeshi.

Rais wa Benin Boni Yayi, mpatanishi wa ECOWAS kwa Burkina Faso, pia yuko ziarani mjini Ouagadougou. Lengo la mkutano huu, amesema Rais Boni Yayi, ni " kuafikiana kuhusu namna ya kurudisha taasi za mpito katika uongozi wa nchkulingana na Katiba ya nchi ", " kuachiliwa huru kwa rais na mawaziri wanaoshikiliwa mpaka sasa."

Majadiliano yanatazamiwa kuanza kwa kina Ijumaa jioni wiki hii.

Kwenye ndege, Macky Sall, amekua akijaribu kufanya tathmini sahihi ya hali inayoendelea nchini Burkina Faso. Viongozi wa Senegal wanataka wawe makini kwa kile kinachosemwa utakapo wasili ujumbe huo. "Kila kitu kimewekwa kwenye meza ", maafisa waandamizi walio karibu na Rais Macky Sall wameiambia RFI. Macky Sall anataka kukutana na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, mwenyekiti wa ECOWAS na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Kisha hatua ya kufuata itakuwa kukutana na wale waliohusika na mapinduzi, lakini pia viongozi wa mpito, viongozi wa kisiasa na vyama vya kiraia. Yote haya yanaweza kuchukua muda mrefu. Baada ya kukaa kwenye sehemu ya heshima katika uwanja wa ndege, Gilbert Diendéré na Macky Sall walisafiri hadi mji mkuu. " Hatujui ni kwa muda gani tutakua hapa ", wameendelea kusema maafisa walio karibu na Rais Macky Sall.

Je, Rais Michel Kafando bado anashikiliwa au ameachiliwa huru?

Balozi wa Ufaransa jijini Ouagadougou, Gilles Thibault, amethibitisha kwenye Twitter kuachiliwa kwa Rais Kafando, na kusema kuwa "anaendelea vizuri ". " Ninathibitisha kuachiliwa huru kwa Rais Kafando. Yuko nyumbani kwake ", amesema jenerali Diendéré.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa mpito wamekanusha madai hayo ya wanajeshi waliohusika na mapinduzi (CND). Cherif Sy, Spika wa Bunge la mpito, amekanusha kuwa Rais Michel Kafando hajaachiliwa huru. " Ni uongo mtupu. Kwa kweli, Rais, Mheshimiwa Michel Kafando, amehamishwa kutoka ikuluya Kosyam ambapo alitekwa nyara amepelekwa nyumbani ambapo yuko chini ya ulinzi. Haiko huru kwa chochote kile, ikiwemo kujieleza ", amesema Spika wa Bunge la mpito, Cherif Sy.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.