Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano yaibuka Sudani Kusini

Mwanajeshi wa Sudan Kusini katika mitaa ya Malakal, kilomita 500 kaskazini mashariki mwa mji wa Juba.
Mwanajeshi wa Sudan Kusini katika mitaa ya Malakal, kilomita 500 kaskazini mashariki mwa mji wa Juba. REUTERS/James Akena
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Mapigano mapya yamezuka tena katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity nchini Sudan Kusini kati ya jeshi na waasi na zaidi ya watu thelathini wamepoteza maisha.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya yamesabaisha mashirika ya Kimataifa ya kutoa huduma za kibiandamu kuondoka katika jimbo hilo.

Wakati huo huo waasi nchini Sudan Kusini wameitadharisha serikali ya nchi hiyo kwa kile wanachosema kuwa kuna dalili zinazoonyesha kuwepo dhamira ya kutaka ya kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoshiniwa hivi karibuni, hali ambayo wanasema inaweza kuirejesha nchi hiyo kwenye machafuko yaliyodumu muda wa miezi sihirni na moja sasa.

Kauli hii ya waasi inakuja baada yao kusema kuwa hawakufurahishwa na hatua ya rais Salva Kiir kuamuru kuongezwa kwa idadi ya majimbo kutoka 10 hadi ishirini na nane, hatua ambayo ilitangazwa na serikali siku ya Ijumaa iliyopita.

Waasi wamesema ikiwa mambo yatakuwa hivyo basi huenda kipengele kinachohusu mpango wa kugawana madaraka kuanzia ngazi za chini hadi serikalini kikavunjika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.