Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea Bissau: serikali mpya yaundwa

Waziri Mkuu mpya wa Guinea Bissau Carlos Correia (kulia), mwenye umri wa miaka 81, na mtangulizi wake aliye futwa kazi Domingos Simoes Pereira, Septemba 17, 2015.
Waziri Mkuu mpya wa Guinea Bissau Carlos Correia (kulia), mwenye umri wa miaka 81, na mtangulizi wake aliye futwa kazi Domingos Simoes Pereira, Septemba 17, 2015. AFP/AFP/Archives
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Serikali mpya imeundwa nchini Guinea-Bissau baada ya miezi miwili ya mvutano wa kisiasa tangu Rais Jose Mario Vaz achukuwe uamzi wa kumfuta kazi Waziri Mkuu Domingos Simoes Pereira katikati mwa mwezi Agosti, kwa mujibu wa amri ya rais iliyotolewa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Timu mpya ina mawaziri 15 na makatibu dola 14 pamoja na Waziri Mkuu Carlos Correia, aliyeteuliwa Septemba 17 na Rais Vaz, lakini nafasi ya wizara ya Mambo ya Ndani na maliasili hazioshikiliwa na mtu yoyote kwa sababu ya kutokubaliana juu ya uchaguzi wa majina, kulingana na sheria ya rais iliyosomwa kwenye vyombo vya habari vya serikali.

Nafasi hizo zimekabidhiwa Kaimu Waziri Mkuu Correia, mwenye umri wa miaka 81, veterani wa mapambano ya uhuru na aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa serikali mara tatu (1991-1994, 1997-1998, 2008).

" Uchaguzi wa wajumbe wa baraza la mawaziri ni wajibu wa Rais na Waziri Mkuu. Inahitaji muungano wa maoni ambayo hayakufikia ukamili wake kuhusu uteuzi wa majina yaliyopendekezwa ", imeandikwa kwenye nakala bila maelezo yoyote.

Mawaziri wapya wengi ni kutoka timu iliyovunjwa mwezi Agosti na wengi ni kutoka chama cha (PAIGC) kilio na viti vingi bungeni, amcho ni chama cha Rais Vaz.

Vyama vya kiraia na vyama viwili wa upinzani PCD na UM pia vimewakilishwa katika serikali mpya. Lakini chama cha PRS, kiliyochukua nafasi ya pili nchini humo) hakina mwakilishi hata mmoja, kwani kimekataa kushiriki katika serikali mpya.

Wizara mbili muhimu zimekabidhiwa wanawake: Bi Adiato Djalo Nandigna (kutoka chama cha PAIGC), ambaeo hadi Jumatatu alikua mshauri wa Rais Vaz, ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi na Bi Aida Injai Fernandes (kutoka vyama vya kiraia) ameteuliwa kuwa Waziri wa sheria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.