COTE D'IVOIRE-UCHAGUZI-SIASA

Côte d’Ivoire: uchaguzi wafanyika kwa amani licha ya kuchelewa

Nchini Côte d’Ivoire, wapiga kura milioni 6.3 wamejitokeza katika vituo mbalimbali kupiga kura kwa uchaguzi wa rais, ambao ni wa kwanza tangu mwaka 2010 na vurugu ziliyosababisha vifo vingi vya watu viliyoibuka baada ya uchugizi uliyokua ukiwaniwa kati ya Alassane Ouattara na Laurent Gbagbo.

Foleni mbele ya kituo cha kupigia kura cha Koumasi mjini Abidjan, wakati wa uchaguzi wa rais nchini Côte d'Ivoire, Oktoba 25, 2015.
Foleni mbele ya kituo cha kupigia kura cha Koumasi mjini Abidjan, wakati wa uchaguzi wa rais nchini Côte d'Ivoire, Oktoba 25, 2015. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Jumapili hi Oktoba 25, miaka mitano baadaye, wagombea saba walikuwa wanawania ikiwa ni pamoja na rais anayemaliza muda wake, Alassane Ouattara. Na zoezi la kupiga kura limefanyika kwa utulivu.

Mapema Jumapili asubuhi katika eneo la Kumasi, mji maarufu Kusini mwa Abidjan, katika kituo cha kupigia kura cha Mondo katika mtaa wa Remblais 1, wapiga kura walikuwepo hata kabla ya kuwasili kwa maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEC), ambao wanasimamia uchaguzi huo. Hapakuwa na wasiwasi kwa kupiga kuraeneo hilo. Kutoka 07:00 asubuhi saa za Côte d’Ivoire, visanduku vya kura, orodha ya za wapiga kura na vifaa vingine vinavyoendana na uchuguzi huo vilikua tayari katika eneo hilo. Na licha ya mvua za kutosha katika mji wa Abidjan, watu walikuwa wamejipanga foleni kwa kwenda kufanya wajibu wao wa kiraia.

Katika eneo la Yopougon, eneo jingine maarufu, katika kituo cha kupigia kura cha Ficgayoa, hali ilikua tofauti kidogo: watu wachache katika vituo vya kupigia kura na hasa ukosefu kamili vifaa vinavyoendana na uchaguzi. Vifaa vipya vya Kiteknolojia vimetumwa eneo hilo kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya uwazi.

Uchaguzi wafanyika kwa amani Daloa

Daloa mji mkubwa ulio Katikati Magharibi mwa Côte d’Ivoire, uchaguzi umefanyika kwa amani. Vituo vyote vya kupigia kura viliyotembelewa na RFI vilifunguliwa mapema. Lakini vituo vingine vilichelewa kufungua.

Hata hivyo, wagombea wote hawakuwakilishwa katika vituo vya kupigia kura.

Wagombea ni akina nani?

Wagombea walikua kumi mwanzoni mwa kampeni za uchaguzi. Jumapili hii, wamebaki saba ambao wanawania urais nchini Côte d’Ivoire, baada ya Charles Konan Banny, Essy na Mamadou Coulibaly kujiondoa katika kinyang'aniro hicho Ijumaa alaasiri, katikati mwa mwezi Oktoba. Wamebaki katika kinyang'aniro hicho wanawake wawili, Henriette Adjoa Lagou na Jacqueline Claire Kouangoua na wanaume watano, Pascal Affi N'Guessan, Siméon Kouadio Konan, Kacou Gnangbo, Bertin Konan Kouadio na Alassane Ouattara.