COTE D'IVOIRE-UCHAGUZI-SIASA

Côte d'Ivoire: Rais Ouattara achaguliwa kwa kipindi cha miaka 5

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara, mwenye umri wa miaka 73, amechaguliwa tena katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliyofanyika Oktoba 25 kwa kipindi cha miaka 5, Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) imetangaza.

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara (kushoto) na Rais wa zamani Konan Bedié, wakati wa mkutano Oktoba 27, 2015 mjini Abidjan.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara (kushoto) na Rais wa zamani Konan Bedié, wakati wa mkutano Oktoba 27, 2015 mjini Abidjan. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa, Ouattara amepata 83.66% ya kura katika uchaguzi ambao kiwango cha ushiriki kilikua 54.63% wakati ambapo upande mmoja wa upinzani ulikua ulitoa wito wa kususia uchaguzi huo. Matokeo yatawasilishwa kwa Korti ya Katiba.

Akipewa nafasi kubwa ya ushindi, Ouattara, ambaye amewekeza uaminifu wake kwa wananchi kutokana na uchumi wake ambao umeonekana kuimarika zaidi, amemshinda mshindani wake mkuu Pascal Affi N'Guessan, mwakilishi wa chama cha FPI kiliyoanzishwa na Rais wa zamani Laurent Gbagbo, ambaye alipata 9.29% ya kura. Upande mmoja wa chama cha FPI kilitoa wito wa kususia uchaguzi kwa niaba ya uaminifu kwa Gbagbo, ambaye hakuwepo katika uchaguzi huo. Laurent Gbagbo anasubiri kuhukumiwa na Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kiwango cha ushiriki (54.63%, sawa na wapiga kura milioni 3.33 kwenye orodha ya waliojiandikisha 6,301,000) kilikuwa mmoja ya changamoto kuu katika uchaguzi huo wakati ambapo wagombea watatu na upande mmoja wa upinzani walitoa wito wa kususia uchaguzi, wakitaja kuwa uchaguzi huo uligubikwa na wizi.

Kwa upande wake, kambi ya Ouattara ikijiamini katika ushindi wake kwa kipindi kingine cha miaka mitano, ilibainisha ushiriki kama kigezo kitachoamuau uchaguzi wenye kuaminika.

Mwaka 2010, kukataa kuutambua ushindi wa Ouattara kulisababisha Côte d'Ivoire kutumbukia katika kipindi cha miezi mitano ya machafukoyaliyogharimu maisha ya watu 3,000.