Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kujadili Hali ya mauaji nchini Burundi

Sauti 15:05
Studi RFI Kiswahili jijini Dar es Salaam
Studi RFI Kiswahili jijini Dar es Salaam RFI/BILALI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaendelea hii leo kwa siku ya pili mfululizo kupitia na kujadili mswada wa Azimio kuhusu Burundi lililowasilishwa na nchi ya Ufaransa mjini New York.Kimsingi, Azimio hilo linasisitizia shutuma za Umoja wa Afrika na Marekani kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, pamoja na kauli uchochezi za Spika wa Seneti, huku likiweka mkazo kuhusu haja ya mazungumzo ya kitaifa na vikwazo kwa wahusika wa machafuko.Kuzungumzia hali ilivyo nchini humo hivi sasa, nimewaalika Abdulakarim Atiki ni mchambuzi wa siasa akiwa jijini Daresalaam nchini Tanzania, lakini pia Bryan Wanyama ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Kibabii kilichoko Bungoma nchini Kenya.Karibu