Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ahutubia bunge kwa mara ya kwanza

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli  30 octobre 2015.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli 30 octobre 2015. REUTERS/Sadi Said
Ujumbe kutoka: Ali Bilali
2 Dakika

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John pombe Magufuli, hii leo kwa mara ya kwanza amelihutubia bunge huku akiahidi kuwa serikali yake itafanya kazi kwa weledi, wakati huu pia akimwapisha waziri mkuu mpya, Majaliwa Kassim Majaliwa.

Matangazo ya kibiashara

Ni sauti yake waziri mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati akila kiapo hii leo mjini dodoma katika ikulu ndogo ya Chamwino, sherehe ambayo mbali na kuhudhiriwa na rais wa Zanzibar na viongozi wastaafu, wabunge na wageni mbalimbali nao walihudhuria.

Baada ya sherehe za kuapishwa kwa waziri mkuu, baadae wabunge walirejea bungeni ambako rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliwahutubia, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo toka alipoteuliwa kuwa rais baada ya uchaguzi wa October 25 mwaka huu.

Kwenye hotuba yake rais Magufuli, aliwashukuru wananchi kwa mara nyingine kwa kumuamini na kumchagua, ambapo ameahidi kuwa kiongozi atakayewatumikia watu wote bila kubagua, na kwamba lengo lake ni kuhakikisha nchi ya tanzania inasonga mebel kimaendeleo.

Rais Magufuli pia kwenye hotuba yake pia akaeleza malalamiko aliyoyapokea kwa wananchi ambayo yeye anaona ni kero kwa wananchi, maeneo ambayo anasema ni lazima yashughulikiwe ipasavyo ili kuleta uaminifu kwa wananchi.

Kuhusu Uchumi rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itakuwa ni serikali ya viwanda itakayosimamia sheria na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unasimama kwa kujenga na kuendelea viwanda ili kutengeneza ajira zaidi.

katika hotuba yake pia, rais magufuli hakuacha kugusia suala la katiba mpya, ambapo amesema atahakikisha serikali yake inasimamia mchakato huo na kwamba safari hii utakamilika kwa wakati.

Rais Magufuli pia akagusia suala la muungano pamoja na hali ya kisiasa visiwani zanzibar ambapo amesema yeye ni muumini mkubwa wa muungano uliopo na kwamba anaamini mgogoro wa zanzibar uliojtokeza unatatuliwa kwa amani.

Kabla ya kuanza kwa hotuba yake bungeni, rais Magufuli alishuhudia vioja vya upinzani ambao walikuwa wakipiga kelele wakati viongozi wa zanzibar walipokuwa wakiingia bungeni bungeni, ambapo baadae spika wa bunge Job Ndugai alilazimika kutumia kiti chake kuwafukuza nje ya ukumbi wa bunge ili kupisha hotuba ya rais kuanza, jambo ambalo upinzani ulitii na kutoka nje.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.