Pata taarifa kuu
MALI-MASHAMBULIZI-USALAMA

Mali: Rais IBK atangaza hali ya hatari

Vikosi vya usalama vya Mali karibu na hoteli Radisson mjini Bamako, Novemba 20, 2015.
Vikosi vya usalama vya Mali karibu na hoteli Radisson mjini Bamako, Novemba 20, 2015. REUTERS/Adama Diarrav
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Baada ya mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu wengi katika hoteli Radisson ya jijini Bamako Ijumaa wiki hii, Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta aliitisha kikako cha dharura cha Baraza la Mawaziri Ijumaa jioni.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mali ametangaza hali ya hatari kwa muda wa siku kumi na siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa heshima ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo.

Serikali ya Mali imetangaza siku tatu ya maombolezo ya kitaifa na hali ya hatari kwa muda wa siku kumi kuanzia Ijumaa jioni wiki hii baada ya mashambulizi ya hoteli Radisson Ijumaa jijini Bamako. Hatua hizi zilichukuliwa katika kikako cha dharura cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa hadi Ijumaa jioni na Rais Ibrahim Boubacar Keïta, ambaye alirejea nchini mwake alasiri akitokea katika mkutano wa nchi za Sahel jijini Ndjamena, nchini Chad.

"Kikao hicho cha dharura cha Baraza la mawaziri kimechukua hatua zifuatazo, amesema Rais wa Mali: kutangazwa hali ya hatari kuanzia leo, Ijumaa usiku wa manane, bendera zitapandishwa nusu mlingoti nchi nzima na katika balozi zetu ugenini, siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumatatu, Novemba 23 saa 6:00. "

Rais Ibrahim Boubacar Keita pia amesema kuwa mashambulizi hayo yaligharimu maisha ya watu 19 (wateja au wafanyakazi wa hoteli), pamoja na zaidi ya washambuliaji wawili. IBK pia amepongeza kazi ya vikosi vya usalama vya Mali na vile kutoka nje.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.