Pata taarifa kuu
UFARANSA-KENYA-AIR FRANCE-UGAIDI

Ndege ya Air France yatua ghafla Kenya

Ndege ya shirika la ndegea la Air France katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi, mjini Mombasa, Kenya, Desemba 20, 2015.
Ndege ya shirika la ndegea la Air France katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi, mjini Mombasa, Kenya, Desemba 20, 2015. © REUTERS/Joseph Okanga
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 3

Ndege ya shirika la ndege la Air France Boeing 777, ambayo ilikua ikitokea Mauritius ikiwa njiani kuelekea Paris imetua kwa dharura usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili katika uwanja wa ndege wa Mombasa nchini Kenya, baada ya ugunduzi wa kifaa kilichodhaniwa kuwa ni bomu.

Matangazo ya kibiashara

Jumapili hii mchana, Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air France ametangaza kwamba tishio hilo lilikua la uongo.

Ndege ya shirika la Air France ililazimika kutua kwa dharura usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mjini Mombasa, nchini Kenya, kufuatia ugunduzi wa mfuko uliodhaniwa kuwa kulikuemo bomu, polisi ya Kenya imesema. Ndege ilikua ikitokea Mauritius ikiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Charles-de-Gaulle mjini Paris.

Wataalam wa kutegua mabomu waliingia kati mara moja na kujaribu tena mchana wa Jumapili hii kuchunguza kama kifaa hicho kilikuwa bomu au la.

"Kifaa hicho kilichodhania kuwa bomu kimepatikana na kimeondolewa katika ndege ya shirika la Air France na bado kinafanyiwa uchunguzi", Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya imetangaza Jumapili mchana kwenye akaunti yake ya Twitter.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air France, Frédéric Gagey, pia amesema kuwa kifaa hicho kilikuwa hakina madhara yoyote na kwamba lilikua tishio la uongo. "Baada ya uchunguzi, imeonekana kuwa ni tishio la uongo (...) kulingana na taarifa ambazo tunazo", Gagey amesema .

Ndege hiyo yenye chapa AF 463 ilikuwa imebeba abiria 459 na wafanyakazi 14. iliondoka Mauritius saa 3:00 usiku saa za Mauritius (sawa na saa 11:00 jioni saa za kimataifa) na ingeliwasili mjini Paris saa 11:00 alfajiri saa za Paris (sawa na saa 10:50 usiku saa za kimataifa). Lakini ilitua ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi mjini Mombasa, katika pwani ya mashariki, saa 6:37 usiku saa za Kenya (sawa na saa 3:37 usiku saa za kimataifa).

"Rubani aliomba kutua kwa dharura baada ya kifaa kilichodhaniwa kuwa bomu kugunduliwa chooni. Maandalizi ya kutua kwa dharura yalifanyika, ndege hiyo ilitua salama na abiria waliondolewa katika ndege hiyo", msemaji wa polisi ya Kenya Charles Owino, amesma.

Kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Joseph Nkaissery, ambaye alitembelea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi, mjini Mombasa, baada ya ndege hiyo kutua, "wapelelezi wanawahoji abiria kadhaa kuhusu kifaa hicho.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.