VATICAN-KRISMASI

Wakristo duniani kote washerehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu

Wakristo wakiimba nje ya Kanisa la Nativity mjini Bethlehemu, ambako maelfu ya mahujaji wamekwenda kusherehekea Krismasi katika mazingira mazito.
Wakristo wakiimba nje ya Kanisa la Nativity mjini Bethlehemu, ambako maelfu ya mahujaji wamekwenda kusherehekea Krismasi katika mazingira mazito. AFP PHOTO/ MUSA AL SHAER

Wakiristo kote duniani, wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi leo Ijumaa, siku ambayo ni muhimu katika Kalenda ya dini hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ni siku ambayo wanaamini kuwa Mwokozi wao Yesu Kristo alizaliwa mjini Bethlehem nchini Israel.

Asuhubi hii Wakiristo wanakwenda Makanisani kumshukuru Mungu na baadaye kurejea nyumbani na kujumuika na familia zao katika siku hii muhimu.

Wengine hutumia siku hii kuwatembelea wagonjwa hospitalini, kuwatembelea yatima na kutoa zawadi na misaada kwa watu wasiojiweza.

Katika mkesha wa Krismasi, kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis amewaambia Wakiristo kuwasadia watu wasiojiweza badala ya kutumia muda huu kutafuta mali na kusherekea kupita kiasi.

Katika mji wa Bethlehem nchini Israel katika ukanda wa Magharibi, mwaka huu eneo hilo limegubigwa na mapigano kati ya Wapalestina na maafisa wa usalama na kusabisha zaidi ya watu 100 kupoteza maisha tangu mwezi Oktoba.

Krismasi ya mwaka huu inakuja pia wakati huu, makundi ya kigaidi hasa Islamic State yakikita mizizi katika nchi za Mashariki ya Kati hasa Syria na Iraq.