Pata taarifa kuu
ALGERIA-UGAIDI

Algeria: "magaidi" 109 wauawa na wengine 36 kukamatwa mwaka 2015

Picha iliyotolewa Januari 16, 2015 na Wizara ya Ulinzi ya Algeria ikionyesha askari wataalam kwa kukitegua mabomu wakichunguzi udongo wa eneo ambapo ulizikwa mwili wa Hervé Gourdel , mtalii kutoka Ufaransa aliyekatwa kichwa na wanamgambo wa kiislamu.
Picha iliyotolewa Januari 16, 2015 na Wizara ya Ulinzi ya Algeria ikionyesha askari wataalam kwa kukitegua mabomu wakichunguzi udongo wa eneo ambapo ulizikwa mwili wa Hervé Gourdel , mtalii kutoka Ufaransa aliyekatwa kichwa na wanamgambo wa kiislamu. AFP/Ministère algérien de la Défense/AFP/Archives
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Jeshi la Algeria liliwaua "magaidi" 109, neno ambalo jeshi limetumia kwa kutaja waislamu wenye msimamo mkali, na kuwakamata wengine 36 katika mwaka 2015, kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya ulinzi iliyotolewa Jumatatu hii.

Matangazo ya kibiashara

Katika mwaka 2015, "magaidi 109 waliangamizwa na wengine 36 walikamatwa, pamoja na kiasi kikubwa cha silaha na risasi vliokamatwa (...), kulingana na ripoti hii.

Miongoni mwa silaha zilizokamatwa "ni pamoja na vitengo 105 vya aina ya Kalashnikov, bastola 21, bunduki 237 , silaha 8 za kurusha makombora, silaha tano za kurusha makombora ziliyotengenezwa kijadi na kiasi kikubwa cha kila aina ya risasi ikiwa ni pamoja na mabomu 182 yaliotengenezwa kienyeji, mabomu 132 ya kutegwa ardhini makombora matano, "kulingana na taarifa ya wizara ya ulinzi.

Ripoti hii haielezi hasara yoyote iliyotokea upande wa jeshi katika kipindi chote hicho.

Askari kumi waliuawa katikati ya mwezi Julai katika shambulizi la kuvizia lililoendeshwa na kundi la kijihadi kwenye umbali wa kilomita 150 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Algeria, Algiers. Ni shambulizi lililosababisha maafa makubwa dhidi ya vikosi vya usalama vya Algeria mwaka 2015.

Katika mwaka 2014, kundi Jla und al-Khilafa ambalo lilitangaza kuungana na kundi la Islamic State (IS) lilimnyonga mtalii kutoka Ufaransa aliyetekwa nyara katika eneo la Kabylie, eneo lenye milima mashariki mwa mji Algiers. Baada ya miezi mitatu ya ya operesheni ya kijeshi ya kuwasaka waliohusika na mauaji hayo, jeshi la Algeria lilitangaza kuliangamiza kundi la kigaidi.

Licha ya kupitishwa kwa miaka kumi iliyopita Mkataba wa amani na maridhiano, uliyolenga kufunika ukurasa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyosababisha vifo vya watu 200,000 katika miaka ya 1990, makundi ya kiislamu bado yanaendesha harakati zao nchini Algeria na yamekua yakilenga hasa vikosi vya usalama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.