LIBYA-IS-MAFUTA

Libya: IS yajaribu kuteka maeneo ya mafuta

Ghala tatu za mafuta zilikua zikiwaka moto, katika kituo cha mashariki mwa Libya, mwezi Desemba 2014.
Ghala tatu za mafuta zilikua zikiwaka moto, katika kituo cha mashariki mwa Libya, mwezi Desemba 2014. © REUTERS/Stringe

Kama nchini Iraq na Syria, kundi la Islamic State (IS) sasa linajaribu kuyateka maeneo ya mafuta nchini Libya. Jumapili asubuhi Januari 3, kundi la IS liliendesha mashambulizi kadhaa dhidi ya vituo vikuu vya mafuta vya al Sedra na al-Ras Lanouf, kaskazini mwa nchi hiyo, na ambapo shughuhuli ya uzalishaji imesimama kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la IS pia linadai kuuteka mji wa Bin Jawad, kilomita 160 mashariki ya ngome yake ya Sirte, ambako mapigano bado yanaendelea.

Katika propaganda zake katika miezi ya hivi karibuni, kundi la Islamic State liliahidi kuyateka maeneo ya mafuta nchini Libya. Jumapili asubuhi kundi hili lilianzisha harakati zake za kuyateka maeneo hayo. Magari kadhaa ya kundi hili yakiwemo wapiganaji waliokua walijihami kwa silaha za kivita yaliondoka katika ngome ya Sirte. Na kisha wapiganaji wa kundi hili walishambulia kwanza kwa kushtukiza mji wa Ben Jawad, eneo muhimu kwa kuelekea katika kituo kikubwa cha mafuta nchini Libya.

Jumapili mchana, kundi la Islamic State lilidai kwenye mtandao kwamba limedhibiti mji wote huo wa pwani. Mji wa Ben Jawad, ambao hauana watu kwa miezi kadhaa sasa, unapatikana kwenye umbali wa kilomita 600 mashariki mwa mji wa Tripoli, kwenye umbali wa kilomita 130 mashariki mwa mji wa Sirte na kwenye umbali wa kilomita 30 kutoka mji wa Nofaliya unaodhibitiwa na kundi la IS. Hata hivyo, na kwa mujibu wa vyanzo vya nchini humo, mapambano yalikua yakiendea tena Jumapili usiku.

Wakati huo huo, mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga yameendeshwa dhidi ya vituo vya mafuta katika miji ya Ras Lanuf na al-Sedra kwa kufungua njia kwa wanajihadi. Kwa mujibu wa viongozi wa Tobruk, wapiganaji wa IS hawakuingia katika mji wa al-Sedra lakini Jumatatu mchana, mapigano makali yalitokea karibu na mji huo. Watu saba ikiwa ni pamoja na wapiganaji wanne wa IS, walinzi wawili wa wanamgambo wanaolinda mitambo hiyo na raia wameuawa katika mapigano hayo.

Ingawa wapiganaji wa kundi la IS wametimuliwa katika miji hiyo miwili, vikosi vya maeneo hayo vinatarajia kuendesha mashambulizi mapya.

Kabla ya vita, vituo vya mafuta,viliosimama kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, vilikua vikiuza nje ya nchi 80% ya mafuta yasiyosafishwa.