COTE D'IVOIRE -DUNCAN-SIASA

Côte d’Ivoire: Duncan ateuliwa kuwa tena Waziri mkuu

Waziri Mkuu wa Côte d’Ivoire Daniel Kablan Duncan (hapa mwezi Novemba 2012) ambaye Jumatano hii Januari 6 amejiuzulu na kuteuliwa kwa mara nyine tena kuwa Waziri mkuu.
Waziri Mkuu wa Côte d’Ivoire Daniel Kablan Duncan (hapa mwezi Novemba 2012) ambaye Jumatano hii Januari 6 amejiuzulu na kuteuliwa kwa mara nyine tena kuwa Waziri mkuu. © AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Rais wa Côte d’Ivoire, Alassane Ouattara, Jumatano hii, amemteua kwa mara nyingine tena Daniel Kablan Duncan kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Bw. Duncan ameteuliwa baaada ya masaa machache ya kujiuzulu pamoja na serikali yake.

Mwishoni mwa mwaka 2015, Rais Alassane Ouattara alisema wazi kwamba serikali mpya imo mbioni kutangzwa.

Kabla ya kujiuzulu Daniel Kablan Duncan, ambaye alimuandikia barua rais Alassane Ouattara akimueleza kwamba heshima na sifa ya mawaziri mbalimbali walioweza kuhudumu chini ya mamlaka yake: "Napenda kuwasilisha barua yangu ya kujiuzulu kama Waziri Mkuu, na ile ya serikali", amesema Daniel Kablan Duncan ambaye amehudumu kama Waziri mkuu tangu Novemba 2012.

Rais Ouattara alipokea barua hiyo na kuishukuru timu nzima ya serikali yake, akimsifu hasa Waziri wake mkuu anayemaliza muda wake kwa "umahiri wake na uongozi wake". "Tunaanza muhula mpya ambao utaonyesha mwanzo mpya kwa utekelezaji wa shughuli za serikali. Ni kazi yako ambayo ilipelekea raia kuwa na imani na sisi", amesema rais Ouatttara, ambaye alichaguliwa hivi karibuni kwa muhula wa pili.

Wadadisi wanasema Daniel Kablan Duncan ameteuliwa kwa mara nyingine kwenye nafasi ya Waziri mkuu kutokana na kazi nzuri alioifanya tangu Novemba mwaka 2012 alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye nafasi hiyo.

Daniel Kablan Duncan anatarajiwa kuunda serikali mpya, lakini haijafahamika iwapo baadhi ya mawaziri waliohudumu katika serikali iliyopita watateuliwa kwa mara nyingine kwenye nyadhifa walizokua wakishikilia.