Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mazungumzo ya amani ya Burundi kuahirishwa, lakini pia Rais Salva Kiir kuomba msamaha wa wananchi wake.

Sauti 21:04

Katika makala hii tumeangazia kuahirishwa kwa mazungumzo ya amani ya Burundi yaliyokuwa yafanyike mjini Arusha nchini Tanzania mwanzoni mwa juma hili, baada ya serikali ya Bujumbura kuelezea kutokuwa tayari kukaa meza moja na upinzani, wakati Umoja wa Afrika ukiendelea kushinikiza kupelekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani kulinda ussalama wa raia nchini humo.Huko Sudan kusini, rais Salva kiir aliwateua wabunge 50 katika baraza la mawaziri; hatua ambayo ilikaribishwa kuwa mwanya wa kuelekea uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.Lakini katumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wake msamaha kutokana na mateso waliyoyapitia tangu kuanzishwa mapigano mwaka 2013Ni Juma la kumbukumbu ya mauaji ya waandishi wa habari wa jarida linalochapisha vibonzo la Charlie Hebdo, mjini paris Ufaransa, ambapo rais wa nchi hiyo Francois Hollande aliwaasa wafaransa kuishi katika umoja.Ungana nami Reuben Lukumbuka katika makala hii, karibuni.