AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Pistorius aiomba Mahakama ya Katiba kupinga hukumu dhidi yake

Oscar Pistorius wakati Mahakama ikitoa uamuzi Septemba 12, 2014 mjini Pretoria.
Oscar Pistorius wakati Mahakama ikitoa uamuzi Septemba 12, 2014 mjini Pretoria. AFP/POOL/AFP/Archives

Bingwa wa michezo ya Riadha ya walemavu Oscar Pistorius, ambaye alimuua kwa risasi mpenzi wake mwaka 2013, ameiandikia rasmi Mahakama ya Katiba, Mahakama ya juu ya nchini Afrika Kusini, kupinga hukumu dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Pistorius alipatikana na kosa la mauaji baada ya upande wa mashataka kukata rufaa.

Mwanasheria wa mwanariadha huyo mlemavu, Andrew Fawcett amethibitisha barua hiyo ya mteja wake, akibaini kwamba ana imani kuwa mahakama ya Katiba itachukua uamzi wa kuridhisha kwa mteja wake

"Tumewasilisha maombi kwa ajili ya rufaa kwa Mahakama ya Katiba", Andrew Fawcett, mmoja wa wanasheria wa mwanariadha wa zamani, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Wakati wa kesi yake katika Mahakama ya mwanzo, Pistorius, aliokatwa miguu miguu miwili, alipatikana na kosa la mauaji bila kukusudia na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela mwaka 2014. Lakini Mahakama Kuu ya Rufaa ilirejelea hukumu hiyo na kubaini, Desemba 2015, kwamba Pistorius alihusika na "mauaji". Kwa sasa Pistorius anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela. Hukumu yake bado haijatolewa.