LIBYA-IS-AL-SHEBAB

Wapiganaji wa Al Shabab wa Somalia watolewa wito kujiunga na IS

Nchini Libya, kundi la Islamic State linaendelea kujiimarisha hasa kwa kuomba msaada wa wapiganaji wa kiislamu kutoka nje. Kundi hili linajaribu kwa karibu mwaka mzima sasakuwavuta katika ngome yake ya Sirte, wapiganaji wa kigeni.

Gwaride la wapiganaji wapya wa Al Shabab katika mji wa Afgooye, magharibi mwa Mogadishu, Februari 17, 2011.
Gwaride la wapiganaji wapya wa Al Shabab katika mji wa Afgooye, magharibi mwa Mogadishu, Februari 17, 2011. © KENYA-SECURITY/SOMALIA REUTERS/Feisal Omar/Files
Matangazo ya kibiashara

Tawi la kundi la IS nchini Libya kundi limerusha hewani Jumanne hii video ya Libya, ambapo wanajihadi kutoka Somalia wameongea. wapiganaji hao kutoka Somalia wametolea wito wapiganaji wa Al Shabab kutoka Somalia waliobaki katika upande wa al-Qaeda kumtii kiongozi wa kundi la Islamic State, Abubakar al-Baghdadi.

Huu ni ujumbe uliotumwa na wapiganaji wa Kisomalia wa kundi la Islamic State nchini Libya, kwa wapiganaji wengine waliobaki nchini Somalia. Katika video hiyo, wapiganaji wawili kwanza wanakaribisha kwa lugha za Kiingereza na Somalia wapiganaji wa Kisomalia wa kundi la Al Shebab ambao hivi karibuni walijitenga na Al-Qaeda na kujiunga na Islamic State.

Kwa mujibu wa vyanzo katika kundi la IS, baadhi ya wapiganaji waliojitenga na Al-Qaeda walinyongwa na wapiganaji wa Al Shabab. Nchini Libya, wapiganaji hao kutoka Somalia wamewatishi kuwachukulia adhabu ya Mungu. "Oh Mujahidini nchini Somalia ambao mlikula kiapo cha kumtii kiongozi wa kundi la Islamic State, tunawapongeza, tunawapenda kwa jina la Mwenyezi Mungu", amesema mmoja wao. "Kwa wale wa Mujahidini wanaoendelea kuliunga mkono kundi la Al Shabab, tunawatolea wito kujiunga na kundi la Islamic State, laikini mumuogope Mwenyezi Mungu kama mlimwaga damu ya wale ambao walikula kiapo kwa kumtii kiongozi wa kundi la Islamic State ".

Idadi ya wapiganaji wa Al Shabab kutoka Somalia waliojiunga na kundi la Islamic State bado ni ndogo, lakini idadi haiyo haijulikani kama vile wale ambao walijiunga na tawi la IS nchini Libya. Lakini nchini Libya, pembezoni mwa ngome ya Sirte, wapiganaji wa kigeni ni wengi zaidi, kwa kuanzia kwa raia wa Sudan, lakini pia raia wa Tunisia. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wapiganaji hao wa kigeni wanakadiriwa kuwa kati ya 1000 na 1500, kwa jumla ya wapiganaji 3000 wa kundi la IS nchini Libya, chanzo kijeshi cha kijeshi cha Ufaransa kimebaini.