Wananchi visiwani Zanzibar kuadhimisha miaka 52 ya mapinduzi, lakini pia majeshi ya DRC kutakiwa kuondolewa Jamhuri ya Afrika ya kati

Sauti 21:22

Katika makala ya mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii, tunaangazia matukio muhimu yaliyojitokeza kwa juma hili nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako juma hili wabunge wa mkoa wa kivu kaskazini waliomba kufanyike uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya Kijijini Miriki, wakati visiwani Zanzibar wananchi waliadhimisha miaka 52 ya kufanyika mapinduzi, huku nchini Kenya; kinara wa upinzani Raila odinga aliwataja watu wanaohusishwa na ufisadi katika mradi wa eurobond.Kimataifa tumeangazia sakata la kugawanyika kwa viongozi wa dhehebu la kianglikana kuhusu kubariki ndoa ya watu wa jinsia moja.Hatua ambayo inakuja baada ya kulitenga kanisa la Marekani, kwa kubariki ndoa za watu wa jinsia moja.Ungana nami Reuben Kakule Lukumbuka kusikiliza makala hii.