BURKINA FASO-SHAMBULIO

Burkina Faso: uchunguzi waendelea kwa kuondoa mashaka

Askari akiwa nyuma ya utepe wa usalama mjini Ouagadougou, Januari 17, 2016, Burkina Faso.
Askari akiwa nyuma ya utepe wa usalama mjini Ouagadougou, Januari 17, 2016, Burkina Faso. AFP

Uchunguzi umeendelea Jumatatu nchini Burkina ili kujua hali halisi ya mashambulizi ya kigaidi yaliowaua watu 29 jijini Ouagadougou, ambapo jeshi lilitumwa baada ya tukio hilo lenye kiwango cha juu katika taifa hilo dogo la Afrika ya Magharibi.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya watu wamekua wakijiuliza swali kwa nini shambulio kama hilo halikuwahi kutokea wakati wa utawala wa Blaise Compaoré, rais alie n'gatuliwa madarakani mwezi Oktoba 2014 baada ya miaka 27 ya utawala.

Kwa washirika wa karibu Blaise Compaoré, wanahakikkisha kwamba ubora wa Idara ya Ujasusi ambayo ilisaidia vya kutosha kuzuia tishio lolote kutoka nje wakati huo na kufaulu kuvunja visa vingi vya utekaji nyara katika ardhi ya Burkina Faso. Blaise Compaoré ambaye alin'golewa madarakani, na Idara ya Ujasusi iliyotengenezwa kwa kipindi cha miaka 27 ikafutwa. Wao wanaona kuwa ukosefu wa chombo hiki imara umechangia kwa kutokea mashambulizi hayo.

Katika eneo la mashambulizi, wakaguzi, baadhi wakivalia kanzu nyeupe, wamekua wakiendelea Jumatatu hii na kazi yao ya kukusanya taarifa na takwimu. wachunguzi kumi na nane kutoka Ufaransa, ikiwa ni pamoja na majaji na maafisa wa polisi ya mambo ya kisayansi, walikuepo eneo hilo kusaidia vyombo husika vya Burkina Faso.

Raia wa kigeni kumi na nne au 15, ikiwa ni pamoja na mtoto mwenye umri wa miaka tisa, na raia saba au wanane kutoka Burkina Faso ni miongoni mwa wahanga wa mashambulizi yaliozikumba Ijumaa usiku hoteli kadhaa na migahawa mjini Ouagadougou, kwa mujibu wa tathmini tofauti zilizotolewa na Mamlaka ya Burkina Faso. Miili saba ilikua bado haijtambuliwa.

Wizara ya mambo ya Nje ya Ufaransa, kwa upande wake imebaini kwamba watu thelathini waliuawa katika mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na 10 wasiojulikana.

Baada ya mashambulizi hayo, hatua za usalama zimeimarishwa katika mji mkuu pamoja naulinzi mkali katika hoteli kadhaa na maeneo muhimu. Vizuizi vimewekwa katika barabara zinazoingia na kutoka katika miji mikubwa ya nchi hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha usalama.

Shule la Sekondari la Ufaransa la mjini Ouagadougou limefungwa kwa kusubiri usalama kamili.

Kundi la AQMI lenye mfungamano na Al Qaeda lilikiri kuhusika na mashambulizi hayo.

Miili ya wanajihadi watatu imepatikana bila hata hivyo kuweza kuitambuwa, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Simon Compaoré.