BURUNDI-UN-MACHAFUKO

Burundi: Ubakaji, silaha inayotumiwa kwa ukandamizaji?

Wajumbe wa vikosi vya usalama vya Burundi wanatuhumiwa kutenda vitendo vya ubakaji katika katika maeneo ambayo ni kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.
Wajumbe wa vikosi vya usalama vya Burundi wanatuhumiwa kutenda vitendo vya ubakaji katika katika maeneo ambayo ni kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza. AFP/AYMERIC VINCENOT

Suala la matumizi ya kisiasa ya unyanyasaji wa kijinsia limekua gumzo nchini Burundi. Wajumbe wa vikosi vya usalama walihusika na vitondo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia wakati wa operesheni za polisi na jeshi katika maeneo ambayo ni kitovu cha maandamano, kulingana na ripoti ya Tume Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inakwenda sambamba na ushahidi kadhaa tayari umekusanywa na RFI.

Katika ripoti hiyo, Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inatahadhari hasa ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia nchini Burundi. Vitendo hivyo ambavyo vilitekelezwa na vyombo vya usalama wakati wa operesheni za polisi na jeshi, vimeongezeka kutokana na mashambulizi dhidi ya kambi za kijeshi mwezi Desemba.

Cécile Pouilly msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, ameelezea kutokea kwa hali kama hiyo kila wakati. "Vikosi vya usalama vimekua vikiingia katika nyumba za waathiriwa katika maeneo yanayolengwa na ambayo yanaonekana kama yanaunga mkono upinzani", amesema Cécile Pouilly. "Vikosi vya usalama vimekua viwalazimisha wanawake kuondoka katika nyumba, huku vikiwatenganisha na watu wengine kutoka familia zao, na kisha hurudi ndani ya nyumba na wanawake na baadaye kuwabaka au kuwafanyia madhila mengine. "

Lakini kuna uhakika kwamba vyombo vya usalama vinahusika na vitendo hivi?

Wakati wa matukio hayo, maeneo ambayo ni kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza yalikua yalizingirwa na vikosi vya polisi na jeshi, Umoja wa Mataifa umejibu.

"Kuvunja upinzani iwezekanavyo"

Kwa upande wake Waziri wa Haki za Binadamu wa Burundi, amesema jambo hili sio la kisiasa. Lakini Umoja wa Mataifa unasema kuwa waathirika hawakua wakichaguliwa kiholela. "Taarifa ambazo tumepokea zinafanana na zinaonyesha kweli kwamba vikosi vya usalama na ulinzi vinakwenda mbali kwa lengo la kuvunja upinzani katika maeneo hayo", anasema Cécile Pouilly.

"Kwa sasa, hakuna ambaye alishtakiwa kwa uhalifu huu", Umoja wa Mataifa umelaumu, ukitoa wito kwa uchunguzi huru.

Watu wapotezwa na uwezekano wa kuwepo kwa makaburi ya halaiki

Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa pia ina wasiwasi kuhusu ongezeko la matukio ya mateso yanayotendwa na vikosi vya usalama, kukamatwa kwa wingi kwa vijana, kupotezwa kwa vijana na uwezekano wa kuwepo kwa makaburi tisa ya halaiki ambapo moja ya kaburi la halaiki lina miili 100, Umoja wa Mataifa umeongeza.

"Tunachunguza picha za satelaiti ili kuthibitisha kwamba maeneo yaliyochimbwa ni makaburi ya halaiki", Cécile Pouilly amesema.