Habari RFI-Ki

Michuano ya soka kwa wachezaji wanaochezea nyumbani wanaokutana nchini Rwanda 2016 kuleta ushirikiano bora

Sauti 10:09

Katika habari rafiki hii leo tunazungumzia namna ambavyo wananchi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo walivuka mpaka kuingia nchini Rwanda, wengi mashabiki wakifurahia hatua ya viongozi wa Rwanda na Congo kuacha wazi mipaka yao, lakini ushindi wa timu ya Leopards ya DRC dhidi ya Ethiopia (3-0) ulikuja kuongeza furaha zaidi kwa wananchi wa Goma, Bukavu na wakongo waishio ugaibuni nchini Rwanda.Katika makala hii tunaangazia namna ambavyo soka inaweza kuwaleta pamoja wananchi waishio kwenye mataifa yanayoonekana kuhasimiana.Ungana na mwandishi wetu Reuben Kakule Lukumbuka, kusikiliza makala hii.