LIBYA-SERIKALI YA KITAIFA

Libya: serikali ya kitaifa yaundwa

Hapa, Bunge la Tripoli wakati wa kikao cha bunge cha Desemba 16, 2015.
Hapa, Bunge la Tripoli wakati wa kikao cha bunge cha Desemba 16, 2015. © AFP PHOTO / MAHMUD TURKIA

Mwezi mmoja baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa, pande husika katika mgogoro wa Libya zimetangaza Jumanne hii Januari 19, 2016 kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Matangazo ya kibiashara

Serikali hii inaundwa na watu 32 baada ya mazungumzo yaliofanyika kwa muda mrefu. Serikali moja, kwa sasa ndio itakua shirika wa jumuiya ya kimataifa, ambayo ilikua ikitarajiwa kuwa na uwezo wa kusaidia Walibya ili kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikumba nchi hiyo.

Ni muda mrefu, zaidi ya mwaka mmoja wa mazungumzo. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Bernardino Leon, alilazimika kujiuzulu kwenye wadhifa wake wa kabla ya nafasi yake kurejelewa na Mjerumani Martin Kobler. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amekaribisha uamuzi huu wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, na kuliomba Baraza la wawakilishi nchini Libya, Bunge linalotambuliwa na jumuiya ya kimataifa lenye makao yake makuu mashariki mwa Libyai, kuidhinisha hara serikali hiyo.

Baada ya serikali hiyo kuidhinishwa, itakuwa na kipindi cha mwaka mmoja. Mwezi ujao, serikali mpya itawateua wakurugenzi wa taasisi nyeti kama vile Benki Kuu ya Libya, Mamlaka ya kupambana na rushwa na kisha kufanya kazi kwa kutunga sheria kwa kuwateua viongozi wa kijeshi. Na serikali itafanya hilo kwa ushirikiano na Baraza la Taifa, taasisi ambayo hutumika sambamba na utawala, kwa mujibu wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa. Taasisi hiyo inaundwa na wabunge waishio mjini Tripoli.

Mgawanyiko mkubwa

Serikali hii itaendesha majukumu yake mjini Tripoli. Mji mkuu ambao, kwa mwaka mmoja umekua chini ya udhibiti wa serikali na Baraza la wawakilishi visiotambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Serikali hii itasaidiwa na muungano wenye Waislamu wengi uitwayo Alfajiri ya Libya.