Habari RFI-Ki

Ujumbe wa baraza la Usalama la umoja wa mataifa kutembelea Burundi juma hili

Sauti 10:08

Hii leo katika makala ya Habari rafiki tumezungumzia ziara ya wajumbe wa baraza la Usalama kwa nchi ya Burundi juma hili, Ni ziara inayolenga kuishinikiza Serikali ya Burundi kufanya mazungumzo na upinzani chini ya mpatanishi mpya ili kupata mwafaka wa kudumu wa kisiasa.Wananchi wa Burundi wana matarajio gani katika juhudi hizi mpya za Umoja wa mataifa?Ni ziara inayokuja wakati kukifanyika mjadala wa kitaifa mjini Kirundo, ambapo wajumbe kutoka makundi mbali mbali wanashiriki.Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka katika makala hii.