COMORO-UCHAGUZI

Comoro: kampeni za uchaguzi kuanza rasmi Alhamisi

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Comoro imepangwa kufanyika tarehe 21 Februari. Wakati zikisalia siku 30 ya tarehe hii ya mwisho muhimu kwa nchi ya Comoro, kampeni za uchaguzi wa rais na wakuu wa mikoa zinaanza rasmi Alhamisi hii Januari 21.

Rais wa sasa wa Comore Ikililou Dhoinine.
Rais wa sasa wa Comore Ikililou Dhoinine. © AFP PHOTO / Pool / Andrew Burton
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi hii asubuhi, Januari 21, wananchi wa Comore wanaamka wakijianda kusikiliza sera za wagombea mbalimbali katika uchaguzi wa rais na ule wa wakuu wa mikoa.

Siku 30 zimesalia ili wananchi wa Comore wachuwe uamuzi wa kumchagua rais wao mpya. Upande wa wagombea, kila mmoja amejianda vya kutosha kwa kuwafikishia wananchi na wafuasi wake sera zake. Raia wa Comore waishio katika nchi za kigeni wamekua wakiwatumia ndugu zao waishio nchini Comore pesa za mahitaji mbalimbali, lakini pia kuwapa maelekezo ya kupiga kura.

Hata hivyo, baadhi ya wagombea, kama vile Makamu wa Rais anayesimamia kitengo cha Fedha Mohamed Ali Soilihi, jenerali Salim au Mwanasheria Fahmi Said Ibrahim akiambatana na mshirika wake rais wa zamani Sambi wameelewa kwamba ushawishi huu hauwezi kupuuzwa.

Wagombea hao wameanza kutembelea miji mikubwa ya Ufaransa wanakoishi raia wengi kutoka Comore kama vile Saint-Denis mkoani Paris, Marseille na Lyon.