Habari RFI-Ki

Mahakama ya Zimbabwe kuingiza sheria inayopiga marufuku ndoa za watoto wa kike wenye umri chini ya miaka 18

Sauti 09:44

Katika makala hii tumeangazia hatua ya mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe kutoa uamuzi wa kihistoria wa kupiga marufuku ndoa za watoto walio na umri wa chini ya miaka 18, katika uamuzi ambao umeungwa mkono na wanaharakati nchini humo.Mashirika ya kiraia yaliyoshiriki kuwasilisha kesi hiyo kwenye mahakama ya kikatiba, yameeleza kuridhishwa na kufurahishwa na uamuzi huo wa mahakama, ambapo yanasema kuwa ni ushindi kwao na wanawake nchini humo ambao watoto wao walikuwa kwenye hatari ya kuozeshwa chini ya umri.Je msikilizaji hali ikoje hapo ulipo kulingana na janga hili la ndoa za utotoni kinyume na sheria za nchi nyingi zinavyotamka?