TUNISIA-MAANDAMANO

Tunisia: yakumbwa na hali ya sintofahamu

Maandamano katika mji wa Kasserine, katikati magharibi mwa Tunisia, unaoendelea kushuhudiwa makabiliano na polisi, Jumatano, Januari 20, 2016.
Maandamano katika mji wa Kasserine, katikati magharibi mwa Tunisia, unaoendelea kushuhudiwa makabiliano na polisi, Jumatano, Januari 20, 2016. © REUTERS/Amine Ben Aziza

Jumanne, Januari 19, makabiliano na polisi yalisababisha watu kumi na tano kujeruhiwa katika mji wa Kasserine, katikati magharibi mwa Tunisia. Mapambano yalitokea tena Jumatano katikati mwa mji, wakati ambapo miji mingine imemejiunga na maandamano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Desemba 17, 2010, kifo cha Mohamed Bouazizi kilichotokana na kujichoma moto, muuzaji wa mitaani kutoka Sidi Bouzid, ndio kilikua mwanzo wa "Mapinduzi ya Jasmin" na "maandamano yaliyotokea katika nchi mbalimbali za Kiarabu". Miaka mitano baadaye, Ukanda huu uliorithi kutoka eneo la kijijini katikati magharibi mwa Tunisia, eneo maskini linalokumbwa na ukosefu wa ajira linakumbwa kwa mara nyingine tena na wimbi la maandamano.

Katika mji wa Kasserine, mamia ya watu walikusanyika tena Jumatano hii asubuhi nje ya makao makuu ya jimbo wakidai ufumbuzi wa ukosefu wa ajira, kabla ya kuelekea katikati mwa mji. Waandamanaji walirusha mawe kutokana na hasira, polisi ilijibu kwa kutumia mabomu ya machozi. Askari polisi wanane walijeruhiwa.

Masuala mapana kama ukosefu wa ajira

"Maandamano yalikua makubwa Jumatano ikilinganishwa na siku ya kwanza ya maandamano hayo katika mji wa Kasserine. Kulikuwa na watu wengi kama mara mbili kuliko jana. hali hii imekumbusha matukio makubwa ya 2011.

Kasserine ilishuhudia wimbi la maandamano baada ya kifo, mwishoni mwa wiki iliyopita, cha Ridha Yahyaoui, kijana ambaye hakua na kazi, aliyepoteza maisha alipopanda chuma kiliyokua na umeme mbele ya makao makuu ya jimbo akipinga uamzi wa kumuondoa kwenye orodha ya watu ambao walikua wamepata ajira katika shirika la umma.