UNSCV-BURUNDI-MACHAFUKO

Ujumbe wa UNSC kuwasili Bujumbura leo Alhamisi

Wakati ujumbe wa watu zaidi ya 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ukitarajiwa kuwasili mjini Bujumbura, nchini Burundi Alhamisi hii, Marekani imetoa wito kwa serikali ya Burundi kukubali uchunguzi huru baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kubaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Agosti 20, 2015.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Agosti 20, 2015. AFP/LANDRY NSHIMIY
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inataja kuwepo kwa makaburi ya halaiki, na kuongezeka kwa visa vya mateso na tuhuma za mauaji, ambapo vikosi vya jeshi na polisi vinanyooshewa kidole kuhusika na uhalifu huo. Washington imetoa wito wa kuanzisha mazungumzo ya umoja yasiyokua na masharti kati ya pande zote.

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa MataifaWakati mabalozi unakuja nchini Burundi, kujaribu kuishinikiza serikali ya Bujumbura kushiriki mazungumzo na pande zingine husika nje ya nchi na kutazama jinsi ya kutumwa kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani. Marekani imeelezea wasiwasi wake kuhusu hali inayojiri wakati huu nchini Burundi

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, yenye lengo la kuongeza shinikizo kwa serikali ya Bujumbura kutaka "kuidhinisha kupelekwa kwa haraka waangalizi wa Umoja wa Afrika, ambao watachunguza tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa za haki za binadamu uliyoelezwa katika Ripoti ya Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, na kuacha kuwasumbua waangalizi hao kuendesha shughuli yao".

"Watu wote waliohusika na uhalifu dhidi ya raia wa Burundi watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria", taarifa hiyo imeongeza.

Itafahamika ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utapitia Ethiopia, kabla ya kuelekea Burundi, na utafanya ziara ya siku mbili nchini humo.