Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Uchaguzi mpya wa urais kufanyika visiwani Zanzibar marchi 20 mwaka huu, wanasiasa wa Kenya kuweka tofauti zao kando

Imechapishwa:

Tume ya Uchaguzi visiwani Zanzibar nchini Tanzania, imetangaza kuwa uchaguzi Mkuu mpya utafanyika tarehe 20 mwezi wa tatu mwaka huu.Akitangaza tarehe hiyo mpya, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jecha Salim Jecha aliyefuta uchaguzi wa mwaka uliopita aliwataka Wazanzibari kuendelea kuwa watulivu.Msuluhishi wa umoja wa afrika aliteuliwa hivi karibuni na Umoja huo kuwahamasisha wanasiasa nchini DRCongo Edem Kodjo amekutana na kinara wa upinzani nchini humo, Etienne Tshisekedi huko Brussels Ubelgiji baada ya kukutana na wanasiasa wengine kuhusu maandalizi ya mazungumzo ya kitaifa kama ilivyopendekezwa na rais Joseph kabila.Wanasiasa wa serikali na wale wa upinzani nchini Kenya, wameweka tofauti zao kando na kulaani shambulizi la kigaidi dhidi ya wanajeshi wa nchi hiyo lililotekelezwa wiki iliyopita nchini Somalia.Na mengine mengi, ya kimataifa.Ungana nami Reuben Lukumbuka kusikiliza makala hii. 

Sayari ya dunia
Sayari ya dunia