BURKINA FASO-SHERIA

Burkina Faso: kiongozi wa chama tawala cha zamani akamatwa

Eddie Komboïgo, Mei 10, 2015 wakati wa mkutano mkuu wa chama cha CDP.
Eddie Komboïgo, Mei 10, 2015 wakati wa mkutano mkuu wa chama cha CDP. © AFP PHOTO / AHMED OUOBA

Kiongozi wa chama tawala cha zamani, Eddie Komboigo, ambaye alikua alikimbilia uhamishoni amekamtwa Jumamoso Januari 24 mjni Ouagadougou mara baada ya kurejea nchini Ijumaa wiki hii iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Eddie Komboigo anatuhumiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi la mwezi Septemba mwaka uliyopita.

Mwanasiasa huyo anatazamiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria aweze kujibu tuhuma zinazomkabili, siku moja baada ya kurejea katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, baada ya miezi kadhaa ya kutokuwepo. Eddie Komboigo kwa sasa anazuiliwa katika majengo ya polisi. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa chama tawala cha zamani, Komboigo ataohojiwa kabla ya kufikishwa mbele ya jaji. Marafiki zake na watu walio karibu naye watamtembelea Jumatatu, amesema kiongozi huyo.

Eddie Komboigo ni miongoni mwa watu waliokua wakisakwa katika uhusiano na uchunguzi wa jaribio la mapinduzi yalioendeshwa na kikosi cha zamani cha usalam wa rais (RSP). Katika ripoti yake, Kamati ya Uchunguzikuhusu jaribio la mapinduzi imeonyesha, baada ya uchunguzi wake na kusikilizwa kwa mashahidi, kwamba Komboigo alishiriki katika jaribio la mapinduzi.

Alichukua hatamu ya uongozi wa chama, baada ya ya maandamano yaliomn'gomoa rais wa zamani Blaise Compaoré.

Kugombea kwake kwenye uchaguzi wa rais na wa wabunge kulifutiliwa mbali mwezi Novemba mwaka jana na Baraza la Katiba, kufuatia sheria mpya ya uchaguzi. Sheria ambayo inawafuta wale wote waliochangia kwa kujaribu kufanya marekebisho ya Katiba yaliyosababisha kuzuka kwa maandamano ya raia.