MALI-USWISI-AQMI

Mali: AQMI yakiri kumteka nyara raia wa Uswisi Beatrice Stockly

Raia wa Uswisi  kitaifa Beatrice Stockly, Aprili 24, 2012 katika mji wa Ouagadougou, Burkina Faso.
Raia wa Uswisi kitaifa Beatrice Stockly, Aprili 24, 2012 katika mji wa Ouagadougou, Burkina Faso. AFP/AFP

Kundi la AQMI lenye uhusiano na Al Qaeda limekiri kuhusika katika utekaji nyara wa raia wa Uswisi Januari 7, kaskazini magharibi mwa Mali na kuomba wapiganaji wake wanaozuiliwa waachiwe huru kwa sharti la kumuokoa mateka huyo.

Matangazo ya kibiashara

Uswisi kwa upande wake imeomba Jumatano hii kuachiwa huru kwa raia wake "bila masharti ".

Beatrice Stockly ameonekana kwenye video iliyokabidhiwa Jumanne hii jioni kwa shirika la habari la kibinafsi la Mauritania Al-Akhbar, karibu wiki tatu baada ya mwanamke huyo kutekwa nyara. Mswisi huyo ni mtu wa kwanza kutoka nchi za Magharibi nchini Mali kutekwa nyara tangu waandishi wa habari wawili wa RFI kutoka Ufaransa, Ghislaine Dupont na Claude Verlon kuuawa na watekaji nyara Novemba 2, 2013 katika mji Kidal (kaskazini mashariki mwa Mali).

Katika video iliyotazamwa na shirika la habari la Ufaransa AFP Jumatano hii, akivaa mjitandio mweusi, Beatrice Stockly anasema alitekwa nyara Januari 7 katika mji wa Timbuktu, ambako aliishi kwa miaka mingi, akisisitiza kuwa aliongea Januari 19, baada ya mashambulizi ya jijini Ouagadougou yaliyoukumba mji mkuu wa Burkina Faso siku ziliyotangulia, mashambulizi ambayo yalidaiwa kutekelezwa na kundi la AQMI.

"Sisi, Al-Qaeda katika Ukanda wa Maghreb wa Kiislamu, tunakiri kumteka nyara muhubiri huyo wa Kikafiri, Beatrice Stockly, ambaeo kwa kazi yake aliwaondoa watu wengi katika dini ya Uislamu", msemaji wa kundi hili aliyekuwa amevaa sare ya jeshi, amesema kwa lugha ya kingereza, akisisitiza kuwa ni "jambo ambalo hata jeshi la Ufaransa haliwezi kufanya katika mji huo wa kale."

Akikumbusha kwamba aliwahi kutekwa nyara mwaka 2012 wakati mji wa Timbuktu ulikuwa mikononi mwa makundi ya kijihadi, msemaji wa AQMI amesema kuwa wakati huo moja ya masharti ya kuachiliwa kwake ilikuwa "asirejei katika nchi yoyote ya Kiislamu kuhubiri Ukristo ", ahadi ambayo hakuweza kuheshimu, amesema msemaji wa kundi hilo.