ICC-GBAGBO-BLE GOUDE-SHERIA-HAKI

ICC: Laurent Gbagbo asema hana hatia

Laurent Gbagbo na mwanasheria wake Emmanuel Altit katika ufunguzi wa kesi Alhamisi hii Januari 28, 2015.
Laurent Gbagbo na mwanasheria wake Emmanuel Altit katika ufunguzi wa kesi Alhamisi hii Januari 28, 2015. © REUTERS/Peter Dejong/Pool

Kesi ya Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé imefunguliwa Alhamisi hii, Januari 28, 2016 mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire amekana kutokua na hatia kwa mashtaka yanayomkabili. Laurent Gbagbo na waziri wake wa zamani wa vijana wanashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotekelezwa kufuatia uchaguzi wa rais mwezi Novemba 2010. Wawili hao wanasubiri kesi hiyo kwa miaka kadhaa sasa.

Mamia ya maelfu ya wafuasi wa Laurent Gbagbo na Charles Blé wamewasili mbele ya mahakama kwa ajili ya ufunguzi wa kesi hii muhimu. Fulana mpya zenye picha za watuhumiwa hao wawili zimetengenezwa kwa ajili ya kesi hii. Televisheni kubwa imewekwa mbele ya Mahakama ya ICC kwa minajili ya kuwezesha watu kufuata namna kesi hiyo inavyoendelea.

Awali polisi ya Uholanzi ilikua imewapendekeza wafuasi wa watuhumiwa hao kusalia katika maeneo yaliotengwa katikati mwa mji. "Tunakuja kuwaunga mkono, hatuji kufanya vita", Ben Gneba, profesa kutoka Côte d’Ivoire, ambaye anaishi nchini nchini Uholanzi kwa miaka ishirini sasa, amesema. "Pamoja na marafiki, tunachangia kila mmoja kwa kile anachoweza kwa kukodisha kipaza sauti", Ben Gneba amesema. Wafuasi wa watuhumiwa hao wawili wana matumaini kwamba ujumbe wao utawafikia majaji watakao kuwa wakisiliza kesi hiyo.

"Mpango mmoja"

Charles Blé Goudé, mshirika wa zamani wa karibu wa Laurent Gbagbo anatuhumiwa makosa 4 ya uhalifu dhidi ya binadamu mbele ya Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
Charles Blé Goudé, mshirika wa zamani wa karibu wa Laurent Gbagbo anatuhumiwa makosa 4 ya uhalifu dhidi ya binadamu mbele ya Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. AFP PHOTO / POOL / MICHAEL KOOREN

Ni zaidi ya miaka minne sasa, Laurent Gbagbo akizuiliwa katika gerezani la Scheveningen, karibu sawa na muhula mmoja wa urais nchini Côte d’Ivoire. Laurent Gbagbo alikamatwa nyumbani kwake mwezi Aprili mwaka 2011 na majeshi ya Alassane Ouattara yakisaidiwa na jeshi la Ufaransa, na miezi saba baadaye alisafirishwa Hague kwa ndege ya rais.

Muda mrefu akiwa uhamishoni nchini Ghana, Charles Blé Goudé alikabidhiwa Mahakama ya ICC mwezi Machi 2014. Mwaka mmoja baadaye, mwendesha mashtaka aliamua kuwahukumu wote wawili pamoja kwa kosa la uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotkelezwa wakati wa machafuko yalitokea baada ya uchaguzi wa rais mwezi Novemba 2010, na kusababisha, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, vifo vya watu zaidi ya 3,000.

Upande wa masitaka unasema, watu hao wawili wanadaiwa kupanga na kusimamia, pamoja na wengine, "Mpango wa pamoja" ili kumbakisha Laurent Gbagbo madarakani "kwa njia zote, ikiwa ni pamoja na kufanya uhalifu." Kati ya Novemba 27, 2010 na 12 Aprili 2011, mamia ya raia walishambuliwa, walijeruhiwa, waliuawa, walibakwa na kuteswa na vikosi vya serikali ya Cote d'Ivoire, vikisaidiwa na wanamgambo pamona na mamluki.

Zaidi ya mashahidi mia moja wanatazamiwa kusikilizwa katika kesi hiyo.