Pata taarifa kuu
DRCONGO-MICHEZO

Polisi yawasambaratisha waandamanaji waliokuwa wakisherehekea ushindi wa Leopards

Nahodha wa timu ya taifa ya DRC inayoshiriki michuano ya CHAN nchini Rwanda, Joel Kimwaki akishangilia
Nahodha wa timu ya taifa ya DRC inayoshiriki michuano ya CHAN nchini Rwanda, Joel Kimwaki akishangilia CAF
Ujumbe kutoka: Ali Bilali
2 Dakika

Polisi jijini Kinshasa imewasambaratisha wapenzi wa soka wafuasi wa timu ay taifa jijini Kishasa kwa kuwavurumishia bomu za kutoa machozi wakati walipkuwa wakisherehekea ushinidi wa timu ya Leopards katika michuano ya CHAN iliokuwa ikifanyika huko Kigali nchini Rwanda. Wafuasi hao wa timu ya taifa walikuwa wakiimba nyimbo zinazo mkashifu rais Joseph Kabila.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka jijini Kinshasa zaeleza kuwa polisi wa kuzima ghasia wamesambaratisha watu zaidi ya mia tano kwa kutumia bomu za kutoa machozi na risase hewani. Waandamanaji hao walitawanyika katika barabara mbalimbali huku polisi ikizidisha ulinzi katika barabara kuu.

Vijana wa timu ya taifa Leopards waliibuka washindi kwa mara ya pili kwa kutwa kombe la vijana wanaocheza soka nyumbani CHAN iliokuwa ikifanyika kigali nchini Rwanda kwa kuigalagaza Mali mabao matatu kwa bila.

Mashuhuda wanasema baada ya filimbi ya mwisho, kundi kubwa lilimiminika mjini huku ikifuatiwa na mziki mnene wa honi za watu waliokuwa kwenye magari na kelele za ushindi.

Hata hivyo watu hawakuwawengi kama ilivyokuwa wakati wa ushindi wa leopards na Amavubi wa Rwanda katika mechi ya Robo Fainali.

Mkuu wa Polisi jijini Kinshasa jenerali Célestin Kanyama, alitahadharisha Jumapili wananchi wa jiji la kinshasa kwa kuwatolea wito kudhihirisha furaha zao wakiwa majumbani kwao. Akizungumza katika televisheini ya taifa jenerali huyo aliwaambia wananchi kwamba ikiwa wataelekea katika maeneo ya umma, watashughulikiwa.

Baadhi ya waandamanaji wamesikika wakilalama kuwa wapo katika gereza lililowazi, kwani hawapo huru kudhihirisha furaha yao.

Timu ay taifa ya DRCongo Leopards imekuwa timu ya kwanza barani Afrika kutwaa mara mbili kombe la michuano ya mataifa ya vijana wanaocheza soka la nyumbani maharufu CHAN. Mara ya kwanza Leopard ilitwaa kombe hilo mwaka 2009, ambapo ilikuwa ni msimu wa kwanza kabisa wa michuano hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.