Pata taarifa kuu
MISRI-IS-MAUAJI

Misri: IS yawanyonga "wapelelezi" wawili wa jeshi

Askari wa Misri katika akipiga doria Novemba 11, 2015 katika mji wa Sharm El Sheikh.
Askari wa Misri katika akipiga doria Novemba 11, 2015 katika mji wa Sharm El Sheikh. AFP/AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Tawi la kundi la Islamic State kundi (IS) nchini Misri imerusha hewani picha zinazoonyesha kunyongwa kwa watu wawili wanaodaiwa kuwa "wapelelezi" kwa niaba ya jeshi, wanaopigana katika eneo la Sinai dhidi ya wanajihadi.

Matangazo ya kibiashara

Mfululizo wa picha zilizorushwa Alhamisi hii jioni kwenye Twitter zinaonyesha watu hao wawili wakinyongwa. Mtu wa kwanza ameonyeshwa kama "afisa wa wa Idara ya ujasusi wa kijeshi" na wa pili "afisa wa jeshi anayehusika na ujasusi." Tovuti maalumu ya Marekani Site imehibitisha uhalali wa picha hizo.

Tangu jeshi lilipo mn'gatua madarakani rais Mohamed Morsi mwaka 2013, jeshi na polisi ni vimekua vikilengwa mara kwa mara na mashambulizi ya wanajihadi, hasa kaskazini mwa eneo la Sinaii, ngome ya tawi la kundi la Islamic State (IS) nchini Misri.

Wanajihadi wanachama wa kundi la Islamic State tayari wamerusha hewani video kadhaa ambazo zinaonyesha kuwau kwa risasi kunyongwa kwa kuwakata vichwa "wapelelezi" wanaotuhumiwa kushirikiana na jeshi la Misri au Israel.

Kwa mujibu wa viongoi wa Misri, mamia ya polisi na wanajeshi wameuawa tangu mwaka 2013 katika mashambulizi ya wanajihadi, hasa kaskazini mwa eneo la Sinai.

tawi la kundi la Islamic state (IS) nchini Misri, hivi karibuni, lilidai kuiangusha ndege ya watalii kutoka Urusi ambayo iliangushwa Oktoba 31 katika eneo la Sinai na kusababisha vifo vya abiria 224.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.