Uchaguzi mkuu nchini Uganda, Hatua ya Upinzani DRC kuitisha mgomo wa nchi nzima.

Sauti 21:04

Mamilioni ya waganda walijitokeza kushiriki zoezi la kupiga kura, wiki hii kumchagua rais wao mpya atakayeongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka mingine mitano, uchaguzi ambao umeonekana kugubikwa na matukio kadhaa ya vurugu, unyanyasaji wa kisiasa, huku kinara wa upinzani nchini humo, Kiiza Besigye akishikiliwa na polisi mara kadhaa.Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatazamiwa kutangazwa jioni hii leo jumamosi.Kwingineko nchini DRC wiki hii, upinzani uliitisha mgomo wa nchi nzima wiki hii, kufwatia kile upinzani ulisema kuwakumbuka mamia ya watu waliokufa wakati wa utawala wa marehemu Mobutu, pale walipoitaka serikali ya wakati huo kuiheshimu demokrasia na utawala bora.Pamoja na matukio mengine duniani tuliyoyaangazia, ungana na mtangazaji wetu utasikia mengi katka makala hii ya leo.Karibu.