Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo kuhusu ziara yake katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, nchini Burundi na mashariki mwa DRC, Syria na mchakato wa amani

Sauti 21:09

Katika makala hii wiki hii tunaangazia ziara yake katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon nchini Burundi, ambako alikutana na wakuu wa serikali huku rais Pierre Nkurunziza alimuhakikishia kiongozi huyo kuwa serikali yake iko tayari kufanya mazungumzo na pande zote zinazohusika na mgogoro unolikumba taifa hilo.Baada ya Burundi, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon alitembelea wakimbizi walioko Kitchanga eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, ambako alielezea kuguswa na hali mbaya inayowakabili wakimbizi.Kimataifa pia tumemulika mwafaka uliofikiwa kati ya Marekani na Urusi, kuhusu usitishwaji wa mapigano ya nchini Syria, kuanza kutekelezwa Jumamosi hii.Karibu kujumuika nasi.