UTURUKI-UTURUKI-USHIRIKIANO

Rais wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan ziarani Côte d'Ivoire

Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara (kulia) akimpokea mwenzake wa Uturuki (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Abidjian.
Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara (kulia) akimpokea mwenzake wa Uturuki (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Abidjian. © REUTERS/Luc Gnago

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, yupo Abidjan tangu Jumapili. Anaanza ziara rasmi ya masaa 48 nchini Côte d'Ivoire. Ziara hii ni ya kwanza kwa rais wa Uturuki kwenye ardhi ya Côte d'Ivoire. Ziara ambayo imewekwa kwenye ishara ya uchumi na uwekezaji.

Matangazo ya kibiashara

Ndege ya rais wa Uturuki ilitua saa moja usiku kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Felix Houphouët-Boigny mjini Abidjan. Rais Erdogan na mke wake walipokelewa na rais wa Côte d'Ivoire na mkewe.

Ziara hii ya kwanza rasmi ya Rais Erdogan nchini Côte d'Ivoire inakuja karibu mwaka baada ya ile ya Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara alioifanya katika mji mkuu wa Uturuki Ankara, mwezi Machi 2015. Wakati huo Rais Ouattara aliomba kuzidisha "mara tatu kiwango cha biashara hadi kufikia mabilioni ya dola kwa mwaka 2019-2020."

Côte d'Ivoire ni mshirika wa kwanza wa uchumi wa Uturuki katika nchi zinazoungumza Kifaransa katika Ukanda wa Kusini mwa Sahara na wa tatu katika Ukanda wa nchi za Kusini mwa Sahara. Rais Recep Tayyip Erdogan ameambatana katika ziara hii na ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara wa Uturuki.

Mikataba kadhaa baina ya nchi hizi mbili imetangazwa. Kunasubiriwa ongezeko kubwa la biashara kati ya nchi hizi mbili. Inasadikiwa kuwa kuna hatari kuwepo na ongezeko la makampuni ya Uturuki nchini Côte d'Ivoire.

Tayari mwaka 2015, makubaliano manane yanayohusiana na ushirikiano katika nyanja za diplomasia, elimu, utalii na mafunzo ya kijeshi yalitiliwa saini wakati wa ziara ya Rais Ouattara nchini Uturuki.

Ziara hii ya Rais Erodgan nchini Côte d'Ivoire, hatua ya kwanza ya ziara yake Afrika Magharibi, itakuwa fursa kwa Uturuki kushindia masoko, lakini pia kupanua ushawishi wake katika Ukanda huo.